Leo nimenunua maembe 3 kwa Sh. 10,000/- bila kupenda

Nasema uwongo ndugu zangu? Msema kweli ni mpenzi wa Mungu
 
Shikamoo! kumbe huwa tunajibizana mbovu na baba zetu na mama zetu wakati mwingine hapa JF! mwaka 1988 nilikuwa sijazaliwa.
Hata mie Babu yangu alikuwa hajabalehe kwani leo ni birthday yangu nimetimiza miaka miwili na nusu.
 
Embe tatu au nne?

Unstutapeli sasa
 
Hiii ndio michezo inafanywa na boda boda usiku,ukimpa hela kubwa sahau hurudishi change
 
Hela imekuwa ya kuwa makini nayo sana, hata Hawa wa mikoani tunatuma wengi wanasema hivyo Ili kutapeli, Kuna mmoja anajifanya anauza vitu vya saluni akanimbia nitume hela mzigo upo anitumie nikamwambia nipo njiani nakuja dar ntachukua kesho kufika kesho yake nikimpigia hapokei so wauzaji Sasa hivi wanatamani hela ya kutapeli kuliko kuuza.
 
Nilikuwa kwenye basi morogoro kuja dar wakaja wale wanaouza mahindi dirishani kuuliza bei nikaambiwa 300/= nikachomoa mmoja nikatoa buku nikitarajia nirudishiwe chenchi yangu.Nikashangaa jamaa huyooo anakimbia nyuma ya basi na kupotelea huko waliobaki pale wakaanza kunicheka nimeuziwa mhindi kwa buku dah!
 
Point bof correction,
Kichwa Cha habari kinapaswa kwa, uliondoka baada ya kuhisi kutapeliwa na siyo kuwa ulinunua,

Kisema ulinunua means ilikuwa hiyari yako. Wewe umepigwa.
 
Wasiwasi wako tu mkuu usimfikirie vbaya siku hizi hali ni mbaya hta chenji imekuwa tabu kupta huenda bado anatafuta
 
Oh mbona kuna wa miaka ya Sabini wapo humu wanatukanwa na akina Salary Slip et al ati ni madogo. JF Hii ni bora ikajifia
Matusi yao hayana nguvu sababu wanatukana wakiwa wamejificha nyuma ya hizi ID na keyboards
Nina uhakika ukukikutana nao live hawataweza japo kukutazama machoni😅😅😅
 
Ili wazo niende na kanzu na niwa pale naona lakufanyia kazi ili wasiibiwe watu wengine ngoja natafakari alafu hii kusema chenji shida hapana Massa mawili aisee huyu aliweka dhamira aniibie ila pia nimejifunza kuwa na chenji kamili manake ningekuwa na hela kamili naaamini hii story isingekuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…