covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 8,355
- 20,792
Kila mmoja wetu amepitia jambo fulani ambalo kwa wakati ule aliona kabisa, “hapa sijui nitavukaje.” Kuna waliopitia magumu ya kifedha, afya, familia, kazi, mahusiano, misiba, madeni, au changamoto ambazo hawakuwahi hata kuwaambia wengine.
Lakini cha ajabu ni kwamba tulipenya na kuvuka.
Ukiangalia nyuma unaweza kusema, “Hii haikuwa uwezo wangu, akili zangu , ujuzi wala maarifa ni Mungu tu ndiye aliyenivusha pale.”
Hivyo hapa kila mtu yuko huru kuweka ushuhuda mfupi au neno la shukrani iwe ni jambo ulilopitia hivi karibuni au miaka iliyopita, lakini kila unapolikumbuka unajua kabisa ilivuka kimiujiza tu.
Labda maneno yako yakawa faraja kwa mtu ambaye leo yupo kwenye jaribu lile lile ulilowahi kulipita.
Mimi nashukuru kwa kila nilichopitia, kwa kila nilichopoteza, kwa kila nilichopata, na zaidi kwa yale ambayo nilifikiri yatanimaliza lakini Mungu akanivusha. 🙏
Kifupi Mungu “Umenipendelea...”
🎵 Henrick Mruma ft. Paul Clement – Umenipendelea 2.0
View: https://www.youtube.com/watch?v=lzkkCCXJuBQ