Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Wazungu ni watu wabaya sana, kumbe tambiko ni ibada kama nyingine na mnyama anayechinjwa anatolewa sadaka na analiwa na wote.
Tambiko lilianza kwa kumuweka ng'ombe kwenye matawi ya mti wa Ululambuli, kisha akachinjwa. Alipochinjwa akachunwa ngozi, akatolewa nyama za kifuani, zikatengenezwa mishikaki, sehemu nyingine zikakatwa katwa.
Nyama ikachomwa kuelekea jua linapotoka, maombi yakafanyika, hatukutaja mashetani, wala hatupandisha majini. Tulimwita Mungu ambaye humwita Sebah.
Baada ya kusali na kila mtu kutaja hitaji la moyo wake, ibada ikaisha, tukaanza kuzila zile nyama za kuchomwa kwa furaha.
Kwa kweli nilifurahi sana kufanya ibada ya kikwetu haswa, sio longolongo za kina Carl Peters na walaghai wengine
Lyubha, Wangaluke, Welelo, Mungu, Sebah.