Leo nimesikia wimbo wa "Kenya taifa letu" nimekumbuka mengi

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Kipindi kile KBC ilikuwa moto kama ilivyo clouds leo (Nazungumzia huku mikoani)
Wimbo huu uliimbwa sana na kiasi kwamba kama tusingekuwa tunaimbishwa nyimbo za uzalendo shule ya msingi, ingetuathiri sana kizazi cha wakati huo watanzania.

Chaz Omuga kabisae, Leonard Mambo Mbotela na wengineo ni baadhi ya majina yaliyoshika wengi na ni vigumu kusahau sauti zao za kuburudisha

Nani anakumbuka pomoja nami?Ijapo najua kizazi chetu wengi walikufa na HIV AIDS kwani ndo ilikuwa imepamba moto na condom tu zenyewe hazikuwepo licha ya dawa kutokufikiriwa hata kama zinaweza tokea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule rombo mkuu,tarakea,mashati nk ilikua unatafuta RTD Ili walau usikilize kipindi cha majira hadi unachanganyikiwa,na hutokaa uipate RTD,kila ukizungusha kutafuta stesheni unakutana na KBC,halafu inakubali balaa,full sauti kwenye medium wave utafikiri kuna mnara wao hapo nyuma ya nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Umenikumbusha mbali sana jameni...yaani enzi zile unaanika betri za Everready kwenye jua ili zitumike mara nyingi hadi zinavuja maji maji fulani hivi, kituo kilikua kimoja tu KBC na vipindi maarufu, kwanza sitokaa nisahau Sundowner.
Watu tumetoka mbali, hata internet nilianza na ile tulikua tunatumia dial-up modem, unalipa Kshs 45 (Tshs 1,000) kwa dakika

Wanangu huwa nawasimulia haya mambo ila hawaoni kama issue, wao wanajua WIFI niliyoweka ya internet bila kikomo ya Zuku, wanaunga vifaa vyao mchana kutwa ni videos na games kwa kwenda mbele. Wanatazama movies za Showmax na nyinginezo nyingi tu, nikikumbuka enzi zetu movie ulikua unakutana nayo mara mbili kwa mwezi, kuna jamaa walikua wanakuja usiku na kigali fulani hivi wanaanika kitambaa cheupe kisha wanakiangazia kurunzi inayomulika na kuonyesha filamu kwenye hicho kitambaa.
Hehehe! Unatembea kilomita zaidi ya kumi usiku ukifuata hiyo movie, ila ukijua nyumbani utarudi na kukuta umesubiriwa kupokea kipodo maana hayo mambo hayakua ruksa, tulikua tunatokea na kuingilia dirishani......hehehe haya mambo bana...mum RIP.
 

Bro umenigusa sana hii story, hisusan ni kile kipengele cha HIV/AIDS. Kipindi hicho wakati AIDS inapamba moto, mimi nami ndo nilikuwa katikati ya kipindi cha "Tamaa zitukiazo ujanani". Nilikuwa na hamu sana ya ngono, lkn hapo hapo gonjwa ndo lilikuwa gumzo, linatisha, mabaunsa, masista wa nguvu wanapukutika mpaka unaweza kumbebe kwa mkono mmoja. Kipindi hicho karibu kila nyumba ilikuwa na mahututi ndani. Karibu kila siku watu walikuwa wakizikwa huku wamebakia kilo 2. Kuna kipindi nimerudi likizo wakati niko kidato cha 6. Kuanzia siku ya kwanza ya likizo mpaka namaliza likizo karibu kila siku ni kuzika tu. Muda huo huo majumbani kuna mahututi kibao kama siyo wa Leo basi kesho. Mpaka wakati shule imefungua uncle akaniambia wewe ondoka tu tuachie haya mambo, maana ilikuwa bandika bandua. Mpaka wazazi kipindi hicho wakituona vijana tunapendeza, tukiwa ba miaka kati ya miaka 18 mpaka 25, walikuwa wanalia machozi, wakisema tunajua udongo utawameza wote.
Kweli tunamshukuru Mungu kwamba tulipita kipindi kile. Nawakumbuka sana mabraza na masista wa enzi hizo ambao walikuwa wakila bata kwa kwenda mbele. Ghafla bata likaingia shubiri. Walijikuta wakilazimika kubadili mtindo maisha kabisa bila unafiki wala kupepesa macho. Hata nakumbuka rais wetu kipenzi wa wakati huo aliwahi sema "KITUMBUA KIMEINGIA MCHANGA". Akimaanisha hakuna namna hatupaswi kuendelea kula kitumbua kilichoingia mchanga. Lkn kufanya hivyo haikuwa rahisi. Bado watu waliendelea kula kitumbua licha ya kuingiwa mchanga, hivyo hivyo kwa shida. Katika maana ya kuwa bata ziliendelea, lkn kwa mawazo sana. Mtu akitembea na mwanamke anabakiwa na mawazo. Sijui anao au hana!!!? Raha yoote kwisha. Kitumbua kinamemesuka mchanga ukitafuna. Tukajiona ni wenye mikosi na kunyang'anywa utamu na mtu katili. Kwa ujumla hali haikuwa rafiki. Kipindi kile kilikuwa "you do you die". Tulielewa hivyo.
Hali sasa ni tofauti, hakuna tena mahututi. Watu waliopukutika na kunyauka mpaka ukimuona unaweza ukaogopa. Maendeleo ya kitiba yamepiga hatua kubwa sana.
Lkn changamoto ni kuwa vijana wa kizazi kipya hawauelewi "practically" ukimwi, wanaelewa kwa nadharia tu. Hivyo hawachui tahadhari. Sitashangaa nikisikia kiwango cha maambukizi mapya ni kikubwa kuliko zamani. Inawezekana kwa kuwa vijana hawajui ukimwi unavyonyanyasa na kutesa. Kwa hili ni vyema picha na senema za zamani zikatumika kuwaelimisha. Maana kipindi chetu hizi mbinu zilisaidia kutufanya tuogope ukimwi. Ukimwi ulikuwa unatesa mpaka unaogopewa kuliko muumba. Nasema hivyo kwa maana watu walikuwa wanaogopa kufanya uzinzi na uasherati si kwa sababu ya kutii amri ya Mungu, bali kwa kuogopa ukimwi. Maana kipindi kile ukijifanya kidume umekwenda na maji.
Yangu ni hayo tu kuhusu kumbukumbu ya zaidi ya miaka 25 iliyopita.
 
Enzi hizo nipo chalii mdogo. Sasa Mtaani Demu kisu hatari Akafariki kwa Ngoma. Sasa Kwenye msiba Vijana wenye meno yao zama hizo kila m1 yupo na na huzuni. Kisa Dada aliwachanganya
Sisi tunawaangalia Machoni na kwa kudadisi!
 
Enzi za cinema...lkn sijui km mikoani zilikuwepo mkuu[emoji23][emoji23][emoji23]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Buda.....and you're lucky if you could get kbc English service or else you're stuck with machokaa na "je huu no ungwana?"

R.I.P to your dear Mom.
 
Nime kumbuka wakati ule NYANGAU ZILIKUWA NYANYAU KWELI ZILI POLA NDEGE ZETU BANA DA ! kweli siku zinaenda

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hivyo hamjaanza kunyan'ganywa mindege juzi, ni kitu kilianza tangu enzi za mababu zenu, desturi ya kutolipa madeni ya watu mnazembea, vinachukuliwa.
Hii ya juzi nahisi imewatia adabu, mkulima kajitilia mipesa yake mfukoni kimya kimya, ila natumai mlimlipa ya kutosha kumnyamazisha maana asije akawapa jeuri wengine wote ambao mumegoma kuwalipa.
 
Bwaaaaaahhhhh
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…