Leo nimetafakari sana kifo cha Rais Benjamin Mkapa

Leo nimetafakari sana kifo cha Rais Benjamin Mkapa

Status
Not open for further replies.
BINAADAM MJANJAMJANJA ANAPOTOA MACHOZI YA MAMBA VINATAKIWA VIPIMO MAALUM KUYATAMBUA!
🤔
 
Hivi huwa sielewi watu mnaomuita JPM dikteta Mara anaua upinzan huwa mna sababu zipi,,ukweli ni kwamba upinzan nchin Tanzania unauliwa na wana nchi wenyew ,,wananchi wanaona serikal iliyopo madarakani inafanya kazi nzuri ,,unategemea nin ? Zaid ,,uchaguz wa mwaka 2020 pamoj na changamoto kadhaa ,ukweli utabak kazi ya JPM ya miak 5 ilikuwa lazima CCM ishinde kwa kishindo ,,
UMESOMA MADA LAKINI AU NDO USHAWASHWA SWITCH YA KUSIFIA KILA MADA UNAKURUPUKA KUSIFIASIFIA TU MADA INA MUHUSU MKAPA WEWE UNAINGIZA MAMBO YA JPM NA WAPINZANI ALAFAU PUNGUZA SHOBO MWANAUME KUSIFIA SIFIA HAIPENDEZI
 
UMESOMA MADA LAKINI AU NDO USHAWASHWA SWITCH YA KUSIFIA KILA MADA UNAKURUPUKA KUSIFIASIFIA TU MADA INA MUHUSU MKAPA WEWE UNAINGIZA MAMBO YA JPM NA WAPINZANI ALAFAU PUNGUZA SHOBO MWANAUME KUSIFIA SIFIA HAIPENDEZI
Punguza hasira za kitoto
 
Leo kuna rafiki yangu moja yupo jikoni kabisa kwa meko, tulikuwa tunazungumzia uteuzi wa Waziri Mkuu.

Nikawa namuuliza vipi ikatokea Majaliwa asichaguliwe na Magu???,Je Mwaka 2015 majaliwa alikuwa chaguo namba 1 la magu.

Akasema ngoja nikupe kwanza mkanda nikianza na makamu wa Rais ule mwaka 2015,JPM aliambiwa apeleke majina 3 awe ameyapanga kimtiririko kwa umuhimu.

Anasema,katika list yake jina LA kwanza lilikuwa Dr. Hussein Mwinyi-Jina la 2 kuna jamaa nimesahau Nina lake na Jina la 3 alikuwa Mama samia. Wazee wakamuchagua Mama samia.

Alisema Magu na Dr.Hussein hawajakutana barabarani wana common bond kati yao ambapo watu wengi hawafahamu.
 
UMESOMA MADA LAKINI AU NDO USHAWASHWA SWITCH YA KUSIFIA KILA MADA UNAKURUPUKA KUSIFIASIFIA TU MADA INA MUHUSU MKAPA WEWE UNAINGIZA MAMBO YA JPM NA WAPINZANI ALAFAU PUNGUZA SHOBO MWANAUME KUSIFIA SIFIA HAIPENDEZI
Ulichoandika hapo umeficha ficha kama mwanmke kwanin usiweke wazi ulichokuwa unataka kusema ,,
 
Kuna watu huwa wana majibu tiyari kabla hawajaingia chumba cha mtihani
 
Huenda Ben alikuwa ni kama malaika aliyekuwa akizuia Shetani asiinue pembe zake zaidi!
Mkuu wanasiasa siyo watu wa kuamini. Mkapa RIP alikuwa akiwa jukwaani anasema hili halafu nyuma anafanya hili. Kuhusu la upinzani, mwaka 2015 kwenye uchaguzi yeye ndiye alizunguka nchi karibu nzima akihakikisha wanatangazwa wagombea wa CCM. Alienda Muleba Anna Tibaijuka alikuwa kapigwa watu walikuwa wanamtukana kama mtoto, akaforce atangazwe.
Akatoka hapo akaenda Bukkoba mjini, Kagasheki alikuwa kagalagazwa, Rwakatale kashinda, hawataki kumtangaza, yuko ndani wananchi wakasema watachoma kituo cha polisi na rwakatale akikubali kupokea pesa wanaenda choma nyumba yake. Vioo vikapasuliwa, watu wakaanza jipanga watafute mafuta walipue kituo ndipo ikabidi tu wamtangaze Rwakatale.
Wanasiasa we waace hivi hivi tu.
 
Leo kuna rafiki yangu moja yupo jikoni kabisa kwa meko, tulikuwa tunazungumzia uteuzi wa Waziri Mkuu.

Nikawa namuuliza vipi ikatokea Majaliwa asichaguliwe na Magu???,Je Mwaka 2015 majaliwa alikuwa chaguo namba 1 la magu.

Akasema ngoja nikupe kwanza mkanda nikianza na makamu wa Rais ule mwaka 2015,JPM aliambiwa apeleke majina 3 awe ameyapanga kimtiririko kwa umuhimu.

Anasema,katika list yake jina LA kwanza lilikuwa Dr. Hussein Mwinyi-Jina la 2 kuna jamaa nimesahau Nina lake na Jina la 3 alikuwa Mama samia. Wazee wakamuchagua Mama samia.

Alisema Magu na Dr.Hussein hawajakutana barabarani wana common bond kati yao ambapo watu wengi hawafahamu.
Mbona hyo stor magufuli mwenyew aliisema.
 
Img-1604949193093.jpg
 
Uzi bora kabisa huu. Bwana yule ajitafakari kifo cha Mkapa. Amelikoroga. Mwana kulitaka mwana kulipewa. Panga halijawahi kuwa shosti wa mmiliki. Ukiliacha sebuleni, jambazi atalitumia dhidi ya mmiliki. Auae kwa upanga atakufa kwa upanga.

Wazee wanaojitambua ni hazina, usipoitumia, jiandae kufungua mlango bila funguo.

Sasa funguo ipo udongoni Lupaso, limebaki panga sebuleni. Matokeo yake ni uharibifu. Wenyeviti wa LAAC/PAC /POAC na KUB huenda kwa mara kwanza wakakosekana bungeni kwa taratibu zilizowekwa awali kwamba watoke upinzani huku the Hague ikiandaa court summons za bwana yule kuitwa ICC!

Balozi na nchi majirani zageuka refugees' camps huku taifa likiugua! Raia umuonaye barabarani kakenua meno hacheki na hajijui kama mdomo upo wazi. Akili haina mawasaliano na mwili maana imezidiwa na ukata uliokithiri huku nduguye akiwa muhanga wa vipigo vya polisi bila matibabu wakati wa kampeni za uchafuzi eti ulioitwa uchaguzi.

R.I.P Mkapa. Hukuwa malaika, walau ulitubu hasa ule udhalimu wa Zanzibar 2001.
 
Kinacho nishangaza mimi ni hawa Watawala wetu ,Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere nae aliwahi kukiri Ubovu wa Katiba tuliyo nayo nae mpaka anaondoka Madarakani zaidi ya kusema/kukemea hakuweza kubadili Katiba hii.

Mzee Mkapa nae mpaka anaondoka Madarakani ameona Ubovu wa Tume yetu na Suala la Katiba mpya ,haku badili kitu zaidi ya kusema tu.Sijui ni kwa nini Watawala wengi wanaona mapungufu wakiwa nje ya Utawala
 
Si

Siyo kama rushwa mkuu.bila kumung'unya maneno ile ni RUSHWA na lengo ni kuunga mikono kupitiliza Kwa ukomo.tupo hapa utaona Mungu atujalie uhai
Eti Ali Mwenye miaka 95 ajengewe nyumba!. Tena siyo nyumba ya kawaida ni hekalu!. Ali na Jakaya mimali yote waliyonayo then majumba haya ya uzeeni ni ya kazi gani, au wanavitafutia urithi hadi vitukuu?

Naamini Ile ni rushwa tu ili muda ukifika wakae kimya mtu ajiongezee mihula!

Ben pamoja na mapungufu yake lakini hakutaka upuuzi wa kuongeza mihula, alikuwa kikwazo!
 
Ka
Eti Ali Mwenye miaka 95 ajengewe nyumba!. Tena siyo nyumba ya kawaida ni hekalu!. Ali na Jakaya mimali yote waliyonayo then majumba haya ya uzeeni ni ya kazi gani, au wanavitafutia urithi hadi vitukuu?

Naamini Ile ni rushwa tu ili muda ukifika wakae kimya mtu ajiongezee mihula!

Ben pamoja na mapungufu yake lakini hakutaka upuuzi wa kuongeza mihula, alikuwa kikwazo!
Kabisa
 
Ni miezi takriban minne sasa tangu Rais Mstaafu BWM atutoke. Bila ubishi, Rais Mkapa alikuwa na ushawishi mkubwa ndani ya siasa za CCM, na ni ukweli usio na shaka kuwa outcome ya siasa za CCM za uchaguzi wa mwaka 2015 ambazo yeye alishiriki kikamilifu ndizo leo hii tunaishi kwa consequences zake. Pamoja na hayo nimetafakari sana juu ya kifo chake na kujaribu kufikiria leo angekuwa hai angekuwa na fikra gani au angeshawishi vipi mwenendo wa serikali hii pamoja na chama chake. Nimetafakari sana pia urais wa huyo mheshishimiwa.

1. Ni mwaka 1995,Mkapa achaguliwa kuwa rais, ala kiapo na kisha kusema wapinzani ni mkono mmojawapo katika mikono yake miwili ya kufanya kazi
Mwaka 1995 baada ya kuapishwa pale uwanja wa uhuru, Mkapa atoa hotuba na kulihutubia Taifa, asema Wapinzani ni watu muhimu kwa maendeleo ya Taifa, Asema mawazo mbadala katika nchi ni kitu chanya kwa Taifa na akasema Wapinzani ni kama mkono mmoja katika mikono yake miwili, na kuwa chama chake ni kama mkono wa pili wote wanahitajika kwa ajili ya usitawi wa nchi.

Miaka 25 baade tumepata rais Mwingine, anayeonekana ana nia ya kuua upinzani, anayewaambia wananchi kuwa pindi wakichagua wasimchanganyie, anawaambia wananchi kuwa wakichagua upinzani katika maeneo yao hatopeleka maendeleo!. Hii ndo Tanzania ya leo, tofauti na miaka 25 iliyopita!. Najiuliza je Mkapa angekuwa hai leo hii akashuhudia aliyoshiriki kuyaasisi mwaka 2015 angekaa kimya ndani ya Chama? - Naamini angemwambia John bila kupepesa macho kuwa John hili unalofanya siyo sahihi badilika!

2. Mkapa atoa kitabu ajuta Mauaji ya Zanzibar
Mwaka mmoja au miwili nyuma kabla ya kifo chake rais Mkapa atoa, kitabu, ajuta kwelikweli ndani ya kitabu hicho mauaji ya watu wasio na hatia huko Zanzibar. Mauaji yale yawa mzigo kwenye mtima wake, yamkosesha raha. Miaka 19 baadae, mauaji yanatokea tena, wananchi wa Zanzibar wauawa, wateswa sababu tu ili Tanganyika iweze kuendelea kuweka mtawala inayemtaka huko Zanzibar. Je Mkapa angekuwepo hai, leo hii angemueleza John kitu gani? - Angemwambia John kuwa uko sahihi well done endelea hivyohivyo? au angemwambia John kuwa usirudie makosa niliyofanya mimi mwaka 2001 waachie Wazanzibari wamchague wanayemtaka?

3. Ni Siku chache kabla ya kifo chake, Wastaafu waitwa dodoma kujadili mtu wa kumpa kijiti cha kuongoza Zanzibar, Mkapa naye ahudhuria
Ni siku chache tu kabla ya kifo chake, Mkapa alikuwa na wenzie, Ali, Jakaya John, Shein na Mama Maria, moja ya kitu walichojadili ni mtu wa kumpa uraisi huko Zanzibar. Kitu kiichoniijia kichwani, hivi Mkapa alikubaliana kweli na wenzie wampe mtoto wa Ali uraisi? - Mkapa huyuhuyu ambaye Sumaye anasema kuwa wakati wakiwa madarakani walikubaliana wasiwape watoto wao vyeo ili kuondoa nepotism ndo eti atakuwa alikubaliana na wenzie kuleta na kulea utamaduni wa Kisultani nchini? - Akili yangu inaniambia kuwa Mkapa lazima alikataa hilo wazo, haiwezekani Mkapa huyu anayejuta kutokana na maafa ya kuwapandikizia Wazanzibar mtawala mwaka 2000 eti akubali tena kurudia dhambi ileile iliyopelekea kuuawa Wazanzibari huko Pemba mwaka 2001. Kwa hiyo akili yangu inaniambia kuwa Mkapa hakuwa onboard kwenye wazo la kumfanya Hussein kuwa Sultan huko Zanzibar.

4. Mkapa afariki, hatukutangaziwa na mkuu wa nchi ugonjwa uliomuua
Mkapa afariki, sheria inasema anapofariki kiongozi mstaafu lazima umma utangaziwe na rais aliyeko madarakani, na katika tangazo hilo mtangazaji inabidi aeleze kilichomuua mgonjwa. Sisi kwetu kweli tulitangaziwa msiba, lakini katika tangazo lile hatukuambiwa mgonjwa kafia nyumbani au kuambiwa jina la hospitali husika kama kafia hospitali. Nimetafakari sana kwa nini taarifa hizo hazikuwa kwenye tangazo? - kwa mujibu wa sheria, Umma si ulikuwa na haki ya kujua hizo info?, kwa nini zilikuwa vague sana?

5. Maombolezo yafanyika, Msiba haukuwa na kiongozi high profile kutoka nje ya nchi
Nimetafakari sana hili suala, nikasema kwa nini viongozi wa nchi jirani hawakuja? Nikasema labda ni Korona, lakini nikafikiria tena, Burundi nao sera yao ya korona si ilikuwa kama sisi na ni marafiki wetu wakubwa kwenye ukanda huu? Kwa nini rais mpya Ndaisheye hakuja? Sijapata jibu.

Kama ni Korona mbona basi raisi Museveni baadae alikuja na convoy yae wamevaa mask kwa ajili ya mradi wa Bomba la Mafuta wakati nchini kwake bado wanapambana na Korona? Kwanini baadae kabla ya uchaguzi Mkuu rais wa Burundi alikuja TZ? Mbona na rais wa Malawi alikuja baadae kipindi cha Kampeni?

6. Maombolezo yaendelea na watu waendelea na shughuli zao utadhani hakuna msiba
Nimetafakari sana hili, wakati mwili wa Marehemu umelala uwanja wa Uhuru hapo Dar, hakuna hata siku moja shule za msingi au sekondari au vyuo zilifungwa ili watoto na walimu wakatoe heshima kwa rais wao wa zamani, Lakini John alipokuwa akienda kwenye kampeni katika jimbo la uchaguzi basi shule zitafungwa, watumishi wa serikali watapewa notice ya lazima wahudhurie mikutano yake, Najiuliza serikali ya John ilishindwaje kuwapa ruhusa maalum watumishi wa serikali kwenda kuuaga mwili wa BWM kama heshima kwake? - Sitegemei jibu liwe eti Jumamosi au Jumapili watu wangeweza kwenda kutoa heshima zao za mwisho, hizo kwa wengine bado ni siku za kwenda kwenye ibada!

7. Ben alitaka tume huru ya uchaguzi
Kabla ya kifo chake, ndani ya kitabu chake, Ben ni kama anaungama, kuna kitu anakisema, kinamuuma roho. Anaona wazi kuwa taratibu za chaguzi nchini haziko fair, hazina haki. Ben anataka tume huru ya uchaguzi ili wananchi wachague viongozi wao haki bin haki - Je Ben angekuwa hai leo hii akajionea hii tume ya John na Mahera wake, Ben angesemaje? - Naamini Ben angemwambia John kuwa Mwanangu sasa hii unachofanya umezidisha hatuendi hivyo!! , hebu achana na uharibifu huu haukusaidii wewe wala nchi!

8. Swali moja ambalo bado nahaingaika nalo, JE BEN ANGEUNGA MKONO MOVE YOYOTE YA KUBADILI VIPINDI VYA UTAWALA KWENYE KATIBA? - Hell no, maana huko nyuma amewahi kusimama kidete kumzuia Salmin Amour kubadili katiba kuendelea kuitawala Zanzibar!

Tangulia Ben, Kifo chako kinaniachia maswali mengi kuliko majibu!!!
Mtabaki na "speculations" zenu hizo wakati wenzenu CCM washaanza kujiandaa kwa kampeni za 2025. Mkija kushtuka hata wabunge "handfuls" hamtawapata.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom