Leo nimetembelea hosptali. Hakuna utajiri zaidi ya Afya

Leo nimetembelea hosptali. Hakuna utajiri zaidi ya Afya

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Today early in the morning I visited Ocean Rd kiukweli Hapa Duniani Afya ndo kila kitu.

And Everything is about God's Grace

Inaumiza sana kuona namna watu wanavyopambania Afya kwa Mateso makubwa.

Kama u hai na Mzima ni Jambo la kushukuru maana hapa Duniani twapita tu. Nothing lasts.

Afya ndo utajiri no 1
 
Pamoja na yote, kumbuka tu huu mtaji wa afya kuna siku utaisha...yaani ni mwendo wa kupokezana tu.

Wakati ukifurahia afya yako kuwa imara, kuna mwenzako huko anapambania uhai wake mda huu, lakini itafikia kipindi ambacho wewe utapambania uzima na afya yako wakati wenzako wanagonga chupa mezani.

It's just a cycle!
 
Kama ni jambo la kushukuru mbona kuna watu wanakufa au kuteseka wakiwa na afya zao njema.

Yote uliyoona ni maisha
 
Usipofika maeneo ya hospitali/ gerezani unajisahaulisha sana na kuona maisha umeyapatia kuna watu wanapata tabu sana kuna ndugu zetu wanapata maumivu makubwa sana wako vitandani wanaitetea afya, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kila wakati sadaka zetu tuzielekeze zaidi kwenye kusaidia wenye mahitaji.
 
Mi huwa nashukuru hata kwa maji baridi ya kuoga na kama pressure ipo yanapanda...na uwezo wa kuzungusha mikono na kuoga
Alhamdullilah for everything

Kuna vitu we take for granted sanaa
 
Hakika, ila tukiwa huku mtaani hatushtuki kabisa. Niliwahi kwenda muhimbili kumtizama mtoto alikua kwenye ward ya watoto wenye uvimbe na kansa, subhanAllah baada ya pale nilipata mazingatio makubwa mno hasa kwa sisi wanawake utakuta una mtoto mzima wa afya lakini maneno machafu tunayowatolea ni mtihani na wala hatuana kauli za dhati za kumshukuru Mungu kwa ajili ya watoto
 
Well said mkuu,ishawahi nikuta mwaka juzi kila hospital nikienda naambiwa tatizo jipya anyway mpaka sasa nipo normal kiasi chake nikajua kweli God still loves me..Kamwe usiache kusali
 
Kabisa. Kuna dogo langu ananiambia bro maisha magumu sababu Sina kazi nikamwambia kama una maisha magumu nenda kwanza hospital ukaone wenye maisha magumu.

Una afya ya mwili na akili, unapumua, unalala vizuri.
 
Back
Top Bottom