Miezi kadhaa iliyopita niliweza kuhamia sehemu X kwa ajili ya utafutaji nilifanikiwa kupata site nikaanza shughuli zangu.
Wenyeji wangu wachache walijua Mimi ni msomi niliyehitimu chuo japo sikutaka kujionesha sana kuwa nimesoma.
Walipokuwa wakiniuliza kuhusu ajira nawambia nangoja serikali ikitangaza nitaomba.
Siku ziliendelea na wote waliamini Mimi ni msomi.
Sasa siku ya Jana nimekaa eneo langu la kazi akaja jamaa mmoja kumsalimia rafiki yake ambaye ni jiran yangu katka eneo la kazi tukaanza kupiga story jamaa akaanza kuniuliza kiwango changu Cha elimu Mimi nikamwambia kuwa nilifeli kidato Cha nne kwa kupata daraja la nne la alama 28 jamaa alishangaa sana akaanza kunishauri jinsi ya kuendelea na masomo kwa kutumia hyo elimu na Mimi nikawa namsikiliza tu
Sasa jamaa kumbe alivyotoka kwangu akaenda kuwaelezea majirani zangu kuhusu nilivyofeli kidato Cha nne
Sasa Leo asubuhi nafika kazini nashangaa majiran wananicheka si ndo wakaanza kufunguka wakisema "tulijua wewe ni msomi kumbe ni Form Four failure"
Na wote wanahangua vicheko na maneno ya kejeli wakinirushia Mimi nikanyamaza kimya wakaongea Hadi walipotosheka wakanyamaza.
Sasa hali hii ikanipa kutafakari kuwa kumbe watanzania wanafurahi wakikuona unateseka na wote mkiwa kwenye same level of thinking na hii imenifunza kuficha uhalisia wangu kwa watu wasionijua .
Watanzania wamejifunza roho mbaya kwa sababu ustaarabu na upendo kwenye jamii unajengwa kama dira na falsafa ya jamii katika Taifa . Wakenya wameonyesha jinsi tulivyo na roho mbaya .
Watu wanampenda mtu kwa sababu ya kupata kitu kwako lakini sio vinginevyo .
Tumeangalia clip moja kule Pemba watu wanaandamana wanapinga ujenzi wa Kanisa . Yaani nyumba ya ibada inakataliwa lakini yanajengwa mahoteli ya wazungu na waarabu kuja kustarehe na kufanya vitendo vya kipuuzi kama ulawiti ,ushoga na usagaji na ulevi wa bangi ,madawa na ulafi mwingi na kukaa uchi ufukweni . Hao wanaonekana ni wa maana kuliko Kanisa linalodhibiti upendo ,haki ,kuacha dhambi na kuishi kwa haki na kumcha Mungu kama Manabii akiwemo Kristo Yesu Masihi . Nikaona ni Wazi watanzania wana roho Mbaya na wanaonekana imejijenga sana . Ndani ya inayoitwa nchi moja lakini kuna eneo moja watu hawaruhusiwi hata kujenga wala kuhamia na Kuwa wakazi wala kupiga kura wala kufanya ibada .
Yaani ni bora Wakenya wana utu kuliko Watanzania .
Serikali imeendeleza ufisadi na madaraka huku wakiwa jenga watu Kuwa pesa ndio kitu cha kwanza . Matokeo yake mpaka 2030 watu watatolewa mpaka figo kwa nguvu na kuuzwa ili watu watajirike . Wenye pesa na madaraka ndio kila kitu kwa sasa .
Kwa hiyo usishangae kuona watu wana roho mbaya .
Gwajima ameiomba serikali kuweka mfumo mzuri wa kisheria wa kudhibiti vitendo vya utekaji na kuhakikisha kila mtu anakua salama na sio kupotea lakini cha ajabu ameshambuliwa na kukaripiwa kwa nguvu zote kuliko hata hao wauaji .
Hii ni roho mbaya sana . Wakenya walikuja kusikiliza tu kesi ya Lisu lakini walipigwa sana na akatokea Mzanzibari akasema walitakiwa warushwe wakiwa maiti au wanapuumulia gesi . Yaani WanaCCM wanahamasisha chuki dhidi ya Wakenya amabao Mtanzania akiwa Kenya anaweza kuishi na kujenga kanisa ,nyumba ,msikiti na biashara zako bila kubughudhiwa kama wanavyobunghudhiwa Watanganyika kule Zanzibar .
Yote ni roho mbaya sana halafu cha ajabu watanzania wanaongoza kwa Kuwa na nyumba nyingi za ibada . Misikiti na Makanisa kila kona na vipaza sauti juu lakini watu wana roho mbaya kuliko wanyama .