Haya Maisha wala yasikusumbue, binafsi nilikua kwa shangazi yangu nakula ugali wa shikamoo mpaka nilipotiza miaka 35, ukifikiria umri unachanganyikiwa. Nilikua hapo nikiwa sina mbele wa nyuma, Maisha magumu na hata hela ya vocha sina. Siku niliyofanikiwa kupata chanzo cha kipato nilishukuru sana japo nilichelewa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuanzisha familia ila nashukru mungu sasa ninasonga mbele. Ninachokuambia kazi buti, usiogope kukaa kwa ndugu na wala usiogope umri japo nichangamoto, epuka wizi, unywaji wa pombe, umalaya na tabia za kishenzi maana hujui kesho yako