RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
💼MHADHARA WA KUMI (10)
Yawezekana mwenzetu umekuwa Bosi au utakwenda kuwa Bosi mpya kwenye shirika, kampuni, taasisi, au ofisi fulani. Najua unajua lakini ngoja tukumbushane; Kuna tabia ya baadhi ya wafanyakazi kwenye maofisi, mashirika, makampuni na maeneo mengine ya kazi huwapokea mabosi wapya kwa mbwembwe, nderemo na vifijo huku wakiwa na maslahi yao binafsi.
Asante kwa kuendelea kunifuatilia. Wafanyakazi wa aina hiyo wengi wanalenga kukumiliki na kukuteka akili ili wakuendeshe kisha wanakupa maneno ya umbea;- "Fulani ni mbaya sana" - "Bora umekuja wewe, fulani ana roho mbaya sana" - "Fulani hafai kuwepo kwenye ofisi hii" - "Fulani muhamishe anatukwamisha hapa ofisini".
Usipokuwa makini utaanza kuwachukia baadhi ya wafanyakazi wako bila sababu za msingi. Ewe bosi mpya usisahau yale maneno ya Mh. Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete yasemayo; USIRITHI ADUI WA MTU. Ni kweli, kamwe usinunue ugomvi usiokuhusu, jaribu kupeleleza kwanini wanakwambia hayo meneno, na wakati unafuatilia maneno yao usisahau yale maneno mengine ya Mh. Jakaya Mrisho Kikwete yasemayo; "AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO".
Usichoke kunifuatilia. Unakuta Bosi mpya umeripoti ofisini asubuhi unaletewa supu ya moto. Kabla ya kuanza kunywa hiyo supu unaletewa kuku mzima wa kuchoma na chachandu pembeni. Wakati unajiuliza uanze kunywa supu au uanze kumtafuna kuku wa kuchoma; ghafla unaletewa bahasha iliyojaa noti (hela). Sasa umeshusha pumzi umeshiba supu na kuku unamuuliza sekretari wako; hivyo vyote vimetoka kwa nani? Unajibiwa supu imetoka kwa Afisa mauzo, kuku wa kuchoma ametoka kwa Afisa manunuzi, na bahasha yenye noti (hela) imetoka kwa Mhasibu - unachekelea kweli kweli hujui kuwa tayari washakuzika kwenye kaburi lao.
Zingatia pia hii nukuu ya aliyekuwa Rais wa Burkina Faso, Thomas Sankara alisema; "HE WHO FEEDS YOU, CONTROLS YOU" - Pia kuna maneno mengine ya msanii Harmonise naye kwenye wimbo wake mmoja aliimba; "UNAKUNYWA TU MIPOMBE HUJUI AMELIPIA NANI.
By: RIGHT MARKER-TZ
Mbezi Louis, Dar es salaam,
Septemba 20, 2024.