Mtamba wa Panya
JF-Expert Member
- Aug 6, 2017
- 764
- 1,892
Jana kulikuwa na mechi ya CAF Champions League #CCL baina ya klabu mbili (zote kutokea Angola), GD S. Esperanca dhidi ya Atletico Petroleos.
Hii ilikuwa mechi ya kundi D ambapo "mwisho wa siku" Petroleos walishinda (1-0) kwenye mtanange wa "kukata na shoka".
Kwa vyovyote vile, inaonekana soka la Angola kwa sasa linatawaliwa na "miamba" hii miwili, tofauti na ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.
Nikaikumbuka timu "chuma cha pua" miaka michache iliyopita, naizungumzia Recretivo do Libolo-- najua kwa kulisikia tu jina hili baadhi ya mashabiki wa timu moja hivi(jina kapuni) wameshaanza " kujambajamba" kwa hofu.
Anyway tuendelee, hawa jamaa walikuwa wababe kweli kweli yaani "wazee wa dozi heavy". Kukupiga "goli nyingi kwako" ilikuwa ni "easy" kwao na hata hapa Tanzania walishawahi "kutia maguu" na kuacha simanzi ukijumlisha na majonzi makubwa.
Naimani "watajipanga upya" na kurudi kwenye ubora wao wanaostahili.
Je, wewe unaikumbukaje Recretivo do Libolo, wababe wa Angola?
..
.