Leo ningekufa

Joined
Oct 9, 2017
Posts
23
Reaction score
48
Unaweza usielewe:
LEO nimepita kisimani nikamkuta dada mmmoja akifua. Nikamuuliza eti dada unavijua VISA vya wanawake?? Akajibu kaka niache.

Nikakomaa anijibu… Badala ya kujibu akaanza kupiga mayowe, na kelele za kuomba msaada.. hadi wananchi wenye mapanga, mawe na mishale wakaanza kuja.

Dada huyo alivyoona wanakuja akajimwagia maji mwili mzima. Nikajua leo ndio mwisho wangu, nikajuta sana kutaka kujua kila kitu.

Wananchi wenye hasira walivyofika, wakamwuliza, kuna nini? Akawajibu, nilidumbukia kwenye kisima na huyu kaka ndie amenisaidia!!

Wakanipongeza sana sana kisha wakaondoka.

Yule dada akaniambia, hivyo ndivyo visa vya mwanamke. Anaweza kukuua au kukulinda! So mheshimu mwanamke hata kinafiki, usijifanye jeuri!!!..

Nikaondoka na funzo langu…… Shikamoo wanawake!
 
MBONA wameshika tamaa waje tuwafundishe kubeba zege maisha yasonge,au kuuza machungwa town tunalaza 30 kwa siku grisi inapatikana
 
Kuna watu watakuja wamejaa lakini mkuu nipe uhusiano kati ya picha na hiyo mada..?
 
Vipi hao wawili pichani wamenyimwa tenda ya kupakia koroshow..mbona wameshika tama na huzuni tele..naulza2 mkuu
 
Hii mbona haina uhusiano wowote na hili sakata la korosho linaloendelea.
 
Nilidhani umekoswakoswa na wale jamaa waliopewa dili ya kununua korosho katika jitihada za kuiba korosho kwenye ile ajali
 
Nilidhani umekoswakoswa na wale jamaa waliopewa dili ya kununua korosho katika jitihada za kuiba korosho kwenye ile ajali
Sisi hatuogopi hao ,tulisha dai Uhuru wetu toka zaman ,kwetu tunazaliwa tukiwa tumefuzu mafunzo ya tpdf
 
Huu ni uchokozi kabisaaaaaa.
 
kwa hiyo mkuu wa nchi ni mwanamke?
anaweza kukuteua na mambo yakawa poa na anaweza kukutosa bila sababu ya msingi na ukaisoma namba?
 
Mchana kutwa nimeshinda bila kutabasam, Ila
baada ya kumaliza kuisoma hadith hiii tu
kilichofuata ni hahahahahahaaaaaaaaaaaa!!!!
Asante mjombaa umetisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…