kamanda wa mara
Member
- Oct 9, 2017
- 23
- 48
Unaweza usielewe:
LEO nimepita kisimani nikamkuta dada mmmoja akifua. Nikamuuliza eti dada unavijua VISA vya wanawake?? Akajibu kaka niache.
Nikakomaa anijibu… Badala ya kujibu akaanza kupiga mayowe, na kelele za kuomba msaada.. hadi wananchi wenye mapanga, mawe na mishale wakaanza kuja.
Dada huyo alivyoona wanakuja akajimwagia maji mwili mzima. Nikajua leo ndio mwisho wangu, nikajuta sana kutaka kujua kila kitu.
Wananchi wenye hasira walivyofika, wakamwuliza, kuna nini? Akawajibu, nilidumbukia kwenye kisima na huyu kaka ndie amenisaidia!!
Wakanipongeza sana sana kisha wakaondoka.
Yule dada akaniambia, hivyo ndivyo visa vya mwanamke. Anaweza kukuua au kukulinda! So mheshimu mwanamke hata kinafiki, usijifanye jeuri!!!..
Nikaondoka na funzo langu…… Shikamoo wanawake!