Leo nitakutajia mchawi wako hapa. Ungana nami

Leo nitakutajia mchawi wako hapa. Ungana nami

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Ni kawaida kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kila mtu kuwa na mbaya wake au kwa lugha nyingine tunaita mchawi. Mtu ambaye hufurahia anguko lako, mtu ambaye huumia moyo unapoinuka.
Mchawi mwingine anaadvance mpaka anaamua kutumia ulozi kukukwamisha. Mwingine hutamka maneno mabaya juu yako akiwa peke yake.

Mchawi anaweza akawa;
-Shangazi
-Mjomba
-Kaka
-Dada
-Rafiki
-Mwanafunzi mwenzako
-Mfanyakazi mwenzako
-Shehe mwenzako
-Mchungaji mwenzako n.k n.k.
Sasa je, utajuaje kuwa huyu meenzangu ni mchawi wangu?
Mchawi ataonyesha dalili hizi;

1. Anapenda kuwa wa kwanza kukupongeza pindi unapoinuka.
Mf. Umeshinda ubunge, udiwani, umepata uboss. Yeye hujitahidi kuwa namba moja kukupongeza.
2. Atakupa salamu ya mshtuko pindi mkionana. Kwakuwa moyo wake amekujaza kwa ubaya hataweza kukusalimia comfortably.
3.Wakati mwingine hawezi kukusalimia. Atakununia au atajifanya yuko busy.
4.Ukimwelezea mikakati yako ya mafanikio atakaa kimya kama kapigwa na ganzi au atachomekea mikakati yake yeye ilhali wewe ndiye unayemsimulia.
5.Hawezi kutazamana na wewe uso kwa uso angalau dk moja bila kukimbiza uso wake.
Enendeni kwa amani mkawatambue wachawi wenu.
 
Back
Top Bottom