Leo Ramadhani siku ya tano Afande Sele bado yupo hai. Je, ni kweli Albadiri inaweza kudhuru mtu?

Leo Ramadhani siku ya tano Afande Sele bado yupo hai. Je, ni kweli Albadiri inaweza kudhuru mtu?

Albadiri ilisomwa na KISHKI ili afande Sele afe kabla ya ramadhani lakini bado anaendelea kudunda...
Kishki baada ya kutamka maneno yale aliomba msamaha akidai alitamka kwa jazba akaomba asamehewe
 
Mtu kamtukana Mungu, wao wanaenda kumshitaki kwa Mungu. Inamaana Mungu hakusikia hayo matusi, au ndio wameamua kumfundisha nini cha kufanya? Ngoja tuwaachie wenyewe mambo yao
 
Alisema kabla ya Ramadhan lakini hakusema ya mwaka gani 🤣🤣🤣🤣 hawa ma Shekh wengine shida sana badala ya kumuombea mtu arudi katika njia ya sawa unaenda kuomba afe ili iweje? Ndio maana Mungu si Athumani.
 
Hakika mkuu
Mwenyezi Mungu katika vitabu vyote anakemea kwa ukali mabaya lakini mwisho anakwambia yeye ni Raheem yaani mpole ukitubu ni mwepesi wa kusamehe.

Maana sisi binadamu tunakosa sana mengine hadharani na mengine sirini ila unaomba toba na Mungu ni raheem na hakuna mtu msafi.

Mwenyezi Mungu kaifanya dini nyepesi sana ila sisi binadamu ndio tunaifanya dini kuwa ngumu sana ila Mwenyezi Mungu ni mpole sana kwa kila anayeomba msamaha ndio maana kila siku tunamuomba maana kila siku tunamkosea.
 
KIFO NI AHADI.
Kusoma Al badri NI Jambo jingine na KUJIBIWA NI JAMBO JINGINE.
hapo hata kama haijajibiwa haimaanishi afande sele alikuwa sahihi.
Muda wake utafika
 
Aliomba toba(msamaha kwa Mungu),Mungu ametoa ahadi ya kumsamehe yoyote,atakaye muomba msamaha,Mungu ni mwingi wa kusamehe.
 
Back
Top Bottom