Leo Serikali kulilia fedha za mabeberu, imekwama wapi?

Leo Serikali kulilia fedha za mabeberu, imekwama wapi?

ibesa mau

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2015
Posts
2,109
Reaction score
1,697
Serikali kila siku inajidai ina fedha za kutosha, inakusanya mapato mengi kuliko serikali zote, Leo kimewakuta nini hadi kilio kila kona.

Ni nashauri tokeni hadharani muwaambie wananchi kwamba Yale mliyokuwa mnajimbwambafai kwa wananchi ilikuwa ni uongo na hadaa.

Wachumi walikuwa wanahoji kila siku, iweje uchumi wa nchi ukue halafu maisha ya watu na umaskini uzidi kuongezeka katika jamii.

Ukuaji wa uchumi ni lazima uwe direct proportional to improvement of social wellfair, lakini huu uchumi tunao hubiriwa ni ule unaokwenda kinyume na nadharia za kiuchumi.

Mabeberu wamefunga nut mbili tu vilio vimekuwa vingi, tusubiri watakapoongeza kufungwa nut ya tatu na kuendelea, hao wanao jimbwambafai mitaani vilio nitakuwa vingi.

Mimi nashauri tutulie tu nut zote ziishe ndio tuanze kutoleana matamko ya kuwataka watu kujieleza. Kwa sababu yanayokuja ni mengi na yanamaudhi.

Kabla hata ya Zitto hajajieleza bungeni, nut ya pili imefunguliwa, na tunasubiri matamko ya viongozi, hilo nalo litapita na litakuja jingine tena na tena.

Kwa sababu Marekani akishaanza kujiondoa usitegemee mataifa mengine makubwa ya nchi za ulaya yanaendelea kubaki na ikumbukwe kwamba hatuna uwezo wa kujiendesha bila kutegemea misaada, bajeti yetu zaidi ya 48% inategemea wahisani wa nje.

Ninachoomba tu Marekani asichomoe betri kwa kukataa kutoa misaada eneo la Afya hususani kwenye dawa za kufubaza virus ARV maana hali itakuwa mbaya zaidi.

Kwa mashirika mengi ya Ulaya ndio yanayotusaidia hususan katika suala afya, mashirika kama EGPA, UKAIDS, USAIDS, Boresha Afya, Marie Stopes n.k hakuna mashirika ya kichina wala India yanayotusaidiia katika suala la afya, hao ni wafanyabiashara waliofika kutafuta fedha.

Atleast tumepata pa kuanzia kuhusiana na vifo na mateso ya baadhi ya wapendwa wetu.

Huyu aliyetajwa na FBI kuhusika katika matukio mbalimbali ya kutesa na kukandamiza haki za watu, ndio tuanzie hapo hapo kwa kumtaka atueleze walipo wale waliopotea na wahusika wa matukio ya utesaji.

Tukumbushane kauli ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa " kesho yetu ni nzuri kuliko jana".

Hili la Makonda limetia nchi dosari, kwa kipindi cha miaka 50 tumeishi vizuri bila scandals.Watu wanaojifanya kwenda makanisani kila siku, wanajifanya kulia kwenye madhabau ya Mungu hadi kama si zinatoka puani wakitoka hapo wanaenda kutesa na kuua watu.

Nategemea makanisa ya kilokole (kipentekoste) kutoa tamko kwamba makonda si muumini wao, amelichafua Kanisa la Mungu.
 
Kujimwambafai kutaisha soon baada ya ban kuanza, na hutasikia tena wakiomba omba hadharani maana wataona aibu, labda wampige chini barshte boy! 🙂
 
FB_IMG_1580192713538.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hela yenyewe Trillioni 1, ambayo tunadai tunakusanya zaidi ya hiyo kila mwezi. Hadi bunge linalia tumekosa Trillioni 1
 
Kuna mtu humu Jamvini aliwahi kumtahadharisha Mkuu wa Nchi kuwa makini na kuwafuatilia Mawaziri wawili.
Mawaziri hao Magu aliwaamini lkn na wao walishamjua ni wa namna gani.
Mmoja wao kila akizungumza haachi kumpamba kwa maneno ya kila namna na hata kutumia vifungu ktk vitabu vya Dini. Ajiulize Waziri yule anaficha nn nyuma ya pazia?? Hapa tulikofika kuna mkono wa Waziri yule.
Wapili ni yule ambae tayari ameshamgundua na kumpa stahiki zake. Nae alikuwa akimpamba kwa kila namna na pia amekuwa akitembea na ilani ya chama. Alikuwa akificha nn kwa kisingizio cha ilani??

Bado tutaendelea kuumizwa kwa sababu ya Unafiki wa Watendaji wa Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umetoa Hoja za msingi sana...ngoja wafia lumumba waje tuone ujinga wao ulivyo zidi kutamalaki
 
Yeah ni sahihi
 
Ndio alihusika na kupotea kwa Azory, Saanane na kupigwa risasi Tundu Lissu?
 
umetoa Hoja za msingi sana...ngoja wafia lumumba waje tuone ujinga wao ulivyo zidi kutamalaki
Hawawezi pita hapa Pompeo ameshawaumbua ,wanatafuta pa kujificha sura zao, aibu tupu
 
Watashindwa hata kulipa mishahara hali itakayochochea maandamano kila kona hadi huko makaburini chato,Jiwe asijifanye kuwa anaweza kutawala kidikteta bila kuchukuliwa hatua
 
Back
Top Bottom