Leo siku ya baba Duniani unajivunia nini kwa Baba yako?

Leo siku ya baba Duniani unajivunia nini kwa Baba yako?

He is a good man...I'm super proud kua nae kama mzee wangu,....Nakumbuka siku nimemaliza chuo aliniambia plainly kwamba urithi wako nimeshakugawia sasa utumie uingie shambani (duniani) kupambana and to every step ambayo nakanyaga nikiomba msaada hasa wa kimawazo hajawahi kuniacha.
Kitu kingine pamoja kutengana na bi mkubwa toka 90's lakin hajawahi niambia neno lolote negative kuhusu bi mkubwa
Hongera sana watunze sana wazaziwako
 
Alinisomesha akahakikisha napata kazi nzuri Mungu amrehemu huko aliko naamini yuko Na watakatifu.
 
Alinifunza heshima,bidii na nidhamu
NB; mzee alinifundisha kuweka serious face kwenye mambo yanayohitaji kuweka seriousness
 
Sijui hata niseme nini, anyways hongereni sana washua wote,pia kwa mliopata bahati hata ya kulelewa na baba zenu mshukuruni sana Mungu.

Kitu pekee ninachojivunia kutoka kwake ni kwamba alisababisha nikazaliwa,hayo mengineyo sikubahatika kuyapata hata kwa uchache tu kwasababu Mungu alimpenda mapema zaidi.
Ila,naamini nitakua Baba bora sana.
 
Vingi vingi Sanaa......
Ila kimoja wapo ni kutusomesha wakati baba Yake yeye hakuwahi kumsomesha walau darasa Moja na SI kwamba hakua na uwezo huo ila............

Mwenyezi Mungu azidi kumbariki na kumuongezea pale tulipopunguza inshAllah...🤲
 
Back
Top Bottom