Leo Tanesco itakuwa kuna intern kitengo cha switch ya kukata umeme. Wanakata kila baada ya nusu saa.

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Naamini kabisa leo kuna mtu anapata mafunzo kwa vitendo kwenye kitengo cha kukata umeme hapo Tanesco.

Maana kila baada ya nusu saa wanakata.

Nimekaa hapa nawahesabia tu.
 
Hapo tanesco lazima kuna mpinzani wa serikali ya mama na vile uchaguzi umekaribia anataka serikali ya mama iangukie pua

Asante sana Mkata umeme huku mtaani umerudi nakuomba ukate tena
 
Yaani hata aibu hawana aisee.

Mtu anaoga ana pata kifungua kinywa anakwenda ofisini kutukatia umeme.

Shame.
 
Kama bandari tumeshindwa wakampa mwarabu hii tanesko wanashindwa Nini kumpa mwarabu angarau huu ujinga uishe
 
Tanesco Wilaya ya °Chunya°, Mkoa wa Mbeya wameshindikana Kwa aslimia 100%
[emoji3][emoji3] Wilaya Ya Chunya-Mkoa wa Mbeya- ukatikaji wa Umeme limekuwa janga Kubwa sana Kwa kweli.
Mbaya zaidi, waathirika wakubwa ni wenye "Elution plants", Karasha (Crusher), na migodi ya dhahabu wanaotegemea Umeme kuendeshea shughuli zao. Kwa hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, na Serikali ya Tanzania kiujumla, mapato yanapungua Kwa kuwa uzalishaji wa madini unapungua sababu ya kukatikakatika Kwa Umeme kila wakati (Umeme usio wa uhakika).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…