Leo Tanesco itakuwa kuna intern kitengo cha switch ya kukata umeme. Wanakata kila baada ya nusu saa.

Jana tumeshindwa kuona mpira maana kila baada ya dk 3 wanakata umeme ikabidi nizime tv tu
 
Tanesco ni shirika lililoshindikana,wanakata na kurudisha umeme kila wanapojisikia[emoji706][emoji706][emoji706]
sasa kama msimamizi wao mkuu kikatiba kiasili ni goigoi na zuzu kwanini tu wasifanye watakalo?
 
Huko maji sasa hivi mnapata??

Mara ya mwisho nimefika huko Lodge nzuri unakuta maji kwenye majaba.
Juma Aweso, Waziri wa maji ametokea mkata wilaya ya Pangani.
Mkata kakuna maji , je Chunya yatatokea wapi?

Mbunge wa Chunya na Lupa wasisahau kitu Dodoma 2025.
 
Umeme Wilaya ya Chunya ni sawa na anasa Kwa Sasa.

Umeme kufika Chunya kutoka Mbeya mjini ni Kms 72 ambapo ndipo sub station iliko.

Tunaomba ijengwe sub station ya umeme Matundasi , Chunya ili kumsaidia Saza, makongorosi, Chunya na Songwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…