Leo tarehe 19/08/2021 Bill Clinton amefikisha Miaka 75

Leo tarehe 19/08/2021 Bill Clinton amefikisha Miaka 75

Polycarp Mdemu

Senior Member
Joined
Jun 2, 2019
Posts
165
Reaction score
209
Huyu Jamaa alikuwa Anakubalika sana na watu, Maana wakati wa kipindi cha kwanza cha uraisi wa Clinton, Bunge la Marekani, lilikuwa linamilikiwa na Republican. Hata hivyo, Clinton alimshinda Mgombea Urais kutoka chama cha Republicans Bw. Bob Dole, katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 1996.

Kuna kashfa ambayo Ilidhoofisha Heshima yake na alishakiwa na seneti kwa kusema uongo mbele ya mahakama juu ya Mahusiono yake ya kimapenzi na mwanamke Monica Lewinsky.

Alipoachia Madaraka bajeti ya nchi ilikuwa na ziada ya pesa kwa mara ya kwanza tangu miaka ya 40.

Bill ni moja ya Maraisi watatu walioshika madaraka ya Uraisi wa USA wakiwa na umri mdogo, Wakwanza alikuwa Theodore Roosevelt alishika madaraka akiwa na miaka 42 akafuata John F. Kennedy alishika madaraka akiwa na miaka 43, Bill alishika madaraka akiwa na miaka 46.

Okay, Usisahau Bill Clinton na Mohamed Dewji wamesoma chuo Kimoja Georgetown University kwa nyakati tofauti, Chuo hiki wamepita Notable alumni wa Kutosha, kama
  • Lyndon Baines Johnson ambaye ni raisi wa 36 wa USA,
  • Iván Duque Márquez Rais wa Colombia,
  • Željko Komšić Rais wa Bosnia,
  • Laura Chinchilla Miranda alikuwa rais wa Costa Rica
  • Saad Hariri Waziri mkuu wa Lebanon,
  • Gloria Macapagal Arroyo Rais wa Philippines
  • José Manuel Barroso Waziri Mkuu wa Ureno
  • Mfame Felipe VI wa Uhispania
  • Mfalme Abdullah II wa Nchi ya Jordan
Nadhani tuishie hapa maana nilikuwa naendelea labda Tutamkuta Mwakalebela au Polepole (Joke) [emoji16][emoji16][emoji16]
Jioni Njema wazee.

Polycarp Mdemu

FB_IMG_1629382428369.jpg
 
Namkubali sana huyu mwamba. Alikaribia kabisa kuifuta unemployment Marekani. Kila mtu alikuwa na kazi na pesa
 
Back
Top Bottom