Leo tuizungumzie Tecno Spark 4 Air, toleo la simu hii August 2019

Leo tuizungumzie Tecno Spark 4 Air, toleo la simu hii August 2019

ashomile

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
2,739
Reaction score
2,697
Tecno Spark 4 Air ni simu yenye sifa zifuatazo:-

1. Display: IPS LCD, 6.1 inches

2. OS: Android 9.0 (Pie)
Kwa kuboresha toleo la hivi karibuni la mfumo endeshi na kiolesura cha mtumiaji, mabadiliko murwa na yenye kuburudisha zaidi yanakusubiri uyavinjari.

Wakati huu, huhitaji tena vipodozi, Hali ya Urembo ya Gumzo la Video ya AI itakufanya ung'are kwenye gumzo la video, ambayo inaongeza furaha zaidi unapozungumza na marafiki. Kwa uboreshaji uliobinafsishwa kwa kina zaidi wa Hali ya Mchezo, utapitia uzoefu wa kuvutia wa michezo.

Unda nafasi tupu, ukuzaji michezo, uharakishaji mtandao, uboreshaji wa taarifa na shughuli mpya zaidi zinachangia kuleta uzoefu wa mtumiaji ulio tumbukizi zaidi na wenye upesi zaidi. Shughuli za kimsingi pia zina masasisho muhimu. OTG pia ipo. SPARK 4, daima inajaribu sana kuwapatia watumiaji wetu maisha janja mazuri zaidi.

3. CPU: Quad-core CPU (4x2.0 GHz Cortex-A53)

4. RAM: 2 GB

5. Storage: 32 GB
Inampatia mtumiaji nafasi zaidi ya kuhifadhi picha, muziki, video, na mafaili. RAM ya 2GB inamaanisha uzoefu wa mtumiaji wenye upesi na mtiririko zaidi kwenye mfumo wetu. Kisindikaji cha Misingi Minne cha 2.0GHz kinakuja na utumiaji nishati kidogo na kasi kubwa zaidi ya uendeshaji.

Wakati huu, kufanya shughuli nyingi kwa wakati mmoja kutakuwa rahisi na kwepesi zaidi. Betri kubwa ya 4000mAh inampatia mtumiaji muda zaidi wa kuingiliana na ulimwengu.

6. Camera: Dual 13 MP, 8 MP

7. 4G Lite
Kupitia 4G, daima utakuwa wa kwanza kujua mienendo na habari za hivi karibuni kwenye zama hizi zinazoendelea kwa upesi. Kwa kutumia mtandao wa 4G kwenye SPARK 4, punguza muda wa kusubiri kwa ufanisi unapokuwa unavinjari mitandao ya kijamii au unatazama video, na upate burudani zaidi bila kususbiri.

8.Face Lock
Fungua simu yako kwa upesi kupitia "uchanganuzi wa uso". Rekodi maelezo yako ya uso, SPARK 4 itajifunza na itatambua uso wako unapowasha mwangaza wa simu yako na kuifungua.

Kupitia “Utambuzi wa Macho Yaliyofumbwa” iliyoongezwa upya kwenye toleo la 2.0, huna wasiwasi wa kufungua simu yako unapokuwa unalala au unapokuwa umefumba macho.

9.Rangi
Usanifu mzima hauna madoido, lakini una rangi shupavu. SPARK 4 inasanifu majalada 4 ya nyuma ya upinde wenye rangi - Zambarau Falme/Buluu Likizo/Kijivu Ukungu/Chungwa Changamfu -. Machaguo ya rangi yanayovuta makini yatakufanya uwe na kifaa kisichokuwa na kifani.

Simu hii inapendeza ukiwa nayo mkono kulingana na designer ilotumika kuwa nzuri kama ya Xiaomi redmi note 7 ,hakika hii simu nimeipenda tokea nimeagizwa jana kwenda kuinunua.

Battery zake 6000mAh, 3000mAh inakuwa kwenye simu na betri lingine linakuwa la ziada 3000mAh . Hii simu hakika ni mkombozi wa Tecno.

Ingie wakazi wa Mwanza ingieni Rwagasole Plaza kuna wauzaji hapo au Lumumba Street ,au Nyerere Plaza na wale wa mikoani fikeni kwa mawakala wa simu za Tecno walio karibu yako, bei za simu hizo ni 210k, 215k, 220k kwa 240k. Simu hii inavutia sana toka nimehama Tecno natamani kurudi.

Kwa yeyote mwenye Tecno Spark 4 Air aeleze ubora wake na matatizo yake. Mimi naishia hapa

Wenu Mtiifu,
William - 0677991687 kwa usahuri na matatizo ya simu nitafute kwa namba hiyo.

IMG20191113111312.jpg
IMG20191113111126.jpg
IMG20191113111136.jpg
IMG20191113111326.jpg
spark4_04.png
spark4_08.png
IMG20191113105935.jpg
 
Acheni kutumia Tecno, kampuni Bora za simu toka china ambazo ni most trusted brand world-wide ni Huawei, Oppo na MI, acheni kutumia hayo makopo na toy za TECNO
Binafsi niko Oppo lakini Tecno hii imenivutia kuanzia mwonekano mpaka designed iko poa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]ni watumiaji wa Iphone pekee bhana ndiyo wanaotoa mapovu siyo na wa Samsung sisi hatuwezi kuwasema vibaya wana Android wenzetu hao wa iOS ndiyo zao hizo
Ngoja wanaotumia iPhone na Samsung waje kutoa mapovu.
Nitarudi baadae kusoma vichambo vyao [emoji14][emoji14]
 
Halafu hata Infinix nao naona wamekuja na simu za muundo kama huo,, yaani ni mvurugano tu siku hizi ukiangalia Samsung Tecno na Infinix kwa nje zote zipo sawa tu kasoro nyuma ukisoma majina na internal specifications ndiyo tofauti..
Ila hawa Tecno wanageza sana wamegeza muundo wa Sumsung As
 
Hebu tumia Spark 4 kuipiga Spark 4 au hazina picha nzuri kuliko Oppo.
2GB RAM kwa 32GB ROM si takataka hiyo!..
Hiyo sio simu ya kushtua bora uhangaike na Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro!.
 
Back
Top Bottom