Leo Tujifunze kuhusu wosia: hati yenye nguvu kisheria kuhusu mgawanyo wa mali baada ya kifo.

Leo Tujifunze kuhusu wosia: hati yenye nguvu kisheria kuhusu mgawanyo wa mali baada ya kifo.

Karim Mussa

Member
Joined
May 6, 2019
Posts
25
Reaction score
7
Wosia ni tamko au maandishi ya mtu akiwa hai, yanayoeleza namna mali zake zitakavyogawanywa kwa warithi wake baada ya kifo. Ni nyaraka muhimu ya kisheria ambayo husaidia kuzuia migogoro ya familia na ndugu baada ya msiba.
---

AINA ZA WOSIA KISHERIA:

1. Wosia wa Maandishi – huandikwa na mtamkaji au wakili akiwa hai.

2. Wosia wa Mdomo – hutolewa kwa maneno mtu anapoona dalili za kifo chake.
---

📝 MAMBO MUHIMU KATIKA WOSIA WA MAANDISHI:

Ili Wosia wa maandishi uwe halali, lazima uwe na:
✅ Umri halali – Mtamkaji awe na miaka 18 au zaidi.
✅ Dhamira ya kweli ya kugawa mali.
✅ Orodha ya mali na mgawanyo kwa warithi.
✅ Msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa.
✅ Tarehe, sahihi na mashahidi wasiopungua wawili.
---

📌 UMUHIMU WA KUWA NA WOSIA:

• Huondoa migogoro ya familia baada ya kifo
• Huzuia udanganyifu juu ya mali za marehemu
• Hutoa nafasi ya kuchagua msimamizi wa mali
• Hutunza kumbukumbu ya mali kwa urahisi wa mirathi
---

🧾 WOSIA WA MDOMO UNATHIBITISHWA VIPI?

✅ Mashahidi wasiopungua wanne
✅ Wawili kati yao lazima wawe ndugu wa marehemu
---

KAMA MAREHEMU HAJAACHA WOSIA, ZINGATIA TARATIBU HIZI:

1. Familia iitishe kikao rasmi cha warithi

2. Pendekeza msimamizi wa mali za marehemu

3. Orodhesha mali zote alizoacha marehemu

4. Watoto wote waliopo ndani na nje ya ndoa watambulike

5. Tambua madeni yaliyobaki

6. Msimamizi aliyependekezwa afungue maombi ya mirathi mahakamani
---

🏛️ USAJILI WA KIFO:

✅ Unafanyika ndani ya siku 30 katika ofisi za RITA
✅ Baada ya Kupata cheti cha kifo na kukamilisha mchakato wa ufunguzi wa shauri lako Mahakama hutoa siku 30 za pingamizi.
✅ Baada ya hapo, mali hugawiwa kulingana na Wosia au makubaliano ya familia.
✅ Msimamizi wa mirathi hutoa mrejesho mahakamani.
---

Mahali pa kuhifadhi Wosia wa maandishi:

• Mahakamani
• Kwa Wakili
• RITA
• Mtu asiye mrithi na mwenye kuaminika
---

USHAURI WA KISHERIA:

Kama unamiliki mali, ni busara kuandika Wosia wa maandishi ukiwa hai.
Tafuta msaada wa mwanasheria ili akuongoze kwa usahihi wa kisheria.
---

✍️ Makala hii imeandaliwa na:
Karimu Mussa (Mwanasheria & Mchambuzi wa Masuala ya Sheria)
📞 WhatsApp: 0755 395 572
📧 Email: [email protected]
📚 Tembelea ukurasa huu kila wiki kwa elimu ya sheria inayogusa maisha yako moja kwa moja.
 
Wosia upo kwa wakili.. .wakili office kariakoo...mtoa wosia makazi Chalinze.. Mtoa wosia kafa gafla.....wakili atapataje taarifa hapo ili awai kusimamia wosia wa mwendazake..!!!!
 
Back
Top Bottom