Leo tumeletewa tena Thamsanqa Jantjie mtafasiri feki kutoka Afrika Kusini

Leo tumeletewa tena Thamsanqa Jantjie mtafasiri feki kutoka Afrika Kusini

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Kama mnakumbuka mwaka 2013 kwenye kifo cha Mandela, serikali ya Afrika Kusini ilileta mtafasiri wa Lugha anaeitwa Thamsanqa Jantjie ambae alitia fora kwa ishara za lugha ambazo hazipo Duniani.

Mtafasiri huyo aliletwa na chama tawala cha ANC kutafsiri lugha ya alama kwa viziwi ambapo alitafsiri lugha kwa viongozi wote wakubwa waliozungumza siku hiyo akiwemo Obama.

Leo historia imejirudia huko Dodoma kwenye msiba wa Magufuli ambapo mtafasiri wa lugha ya KIingereza kwenda Kiswahili amekua akizungumza maneno ambayo hayajasemwa na wazungumzaji.

Mtafasiri huyo amekua akiwalisha maneno kwa lugha ya kiswahili wazungumzaji wa Kingereza.

Angalia huu ni mfano tu.

Alaumiwe lwa kusema uongo. Lakini Mimi alinifurahisha. Alinifanya nicheke sana katika siku iliyojaa majonzi!
 
Umenichekesha hii ishu nshakutana nayo sana hasa wanapokuja wahubiri wa kimataifa kwakweli inasikitisha, asa kwa mfano kuna hyo Raisi wa zambia alikuwa anaongea simple english lakini sasa anayetafsiri
 
Kama mnakumbuka mwaka 2013 kwenye kifo cha Mandela, serikali ya Afrika Kusini ilileta mtafasiri wa Lugha anaeitwa Thamsanqa Jantjie ambae alitia fora kwa ishara za lugha ambazo hazipo Duniani.
Aiiiiiiiibu ad infinitum. Kumbe bado tunao vihiyo wengi. Huyu si wangemtupa korokoroni kwa utapeli tu.
 
Ni raia wa nchi gani apokonywe paspoti huyo, au ni Chattle inc?
 
Alizingua sana hadi watu wakaguna akajishtukia eti hakuskia vizuri wakati maneno yako straight forward.
 
Alaumiwe lwa kusema uongo. Lakini Mimi alinifurahisha. Alinifanya nicheke sana katika siku iliyojaa majonzi!
Yupi, huyu wa leo ama yule wa South?

Mimi yule wa South alinifurahisha kwa kutapeli Dunia nzima.

Dunia nzima jamaa alitupiga changa la macho.

Viziwi wakawa hawaelewi kinachoendelea Duniani. Wakasema labda hii ni lugha ya vipofu😂.
 
Back
Top Bottom