Leo umesema neno 'ASANTE' mara ngapi!?

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2017
Posts
9,758
Reaction score
18,431
Swalamaah [emoji1538]

Leo siku imepita kesho pia itaitwa leo ikifika.

Wahenga walisema "Muungwana ni vitendo" je na wewe ni muungwanaa!?

Utajuaje kama wewe ni miongoni mwa jamii ya waungwa?, embu jiulize na hata utuambie leo umesema neno 'asante' mara ngapi?

Mimi sikumbuki nimelisema hili neno mara ngapi ila kwa haraka haraka tu, nilipoamla nimesema 'asante Mungu' nikiwa mishe mishe mchana nilienda kula nikamshukuru yule mhudumu 'asante kwa chakula' nkatoka hapo nikapitia vocha nkasema 'asante' baada ya kupewa vocha na chenchi yangu.

Huyoo hadi nyumbani nimepokewa nmeambiwa pole nkajibu 'Asante'

Wewe je muungwana??

Ila kuna siku nilimwambia mtu 'asante' akanijibu "kwani nimekupa chakula" nilimshangaa nikaishia kumjibu 'asante' huyoo nikaondoka zangu.

Wewe je muungwana umewahi kutana na watu hawa??

Asanteni!.
 
Mimi nina kawaida hata mhudumu wa hotel akitoa vyombo au kuninawisha mikono nashukuru
 
[emoji87][emoji87][emoji87][emoji87][emoji87][emoji87][emoji87]
 
Mimi nina kawaida hata mhudumu wa hotel akitoa vyombo au kuninawisha mikono nashukuru

Jambo muhimu sana hili mkuu, ajabu kuna watu wanaweza kushangaa eti si umelipia.

Kwangu hii ni kama ibada, kumfanya mtu aone katenda jambo la kushukuriwa.

Hakuna jambo zuri kama kushukuru au kushukuriwa mkuu. Endeleza hii tamaduni mkuu na urithishe wengine pia
 
Dah kwa mazingira ya leo kazini kweli sijalitumia hili Neno.
Ila naanza. Asante mtoa post.
 
hilo neno leo sikuwa na pakulitumia, wacha nijishukuru mwenyewe kwa kumaliza siku na majukumu salama. asante mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…