asidanganyike, hiyo habari ya miaka sita haina ukweli wowote. anatakiwa afikirie nje ya mduara. kufunga ndoa ni sehemu tu ya mapenzi. kwani nani hajui sheria za huko majeshini?? lakini mbona wana waume, wana wake, na wana watoto kabla ya muda waliowekewa?
na kwa taarifa zaidi ni kuwa hata weza pata kazi kama ya huyo binti kwa sababu yeye anafuata mwanamke na si kazi- hawata mkubalia. hapo ni huyo mama ndo anaona rafiki yako hafananiii kwahiyo ametumia kigezo cha kazi.
ushauri ninao weza kumpa
1. aongee na huyo dada kuwa wao wataishi kama mke na mume ila ofisini ndo mwanaume hatapata haki za mume. mama akizaa atapata haki za watoto kutoka ofisini. ndoa ofisini itatambulika baada ya hiyo miaka sita
2. akikataa anatakiwa kukubali hiyo hali, hili la kusema amesubiri siku nyingi halitakiwi ktk kuchukua maamuzi ya maisha. amesubri siku nyingi , lakini hajui ni siku ngapi zimebaki, na zina uzito gani ukilinganisha na hizo zilizopita