Leoni siku ya 362 hivi ile robo tuliyoisomaga ilishapita au bado?

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Wajuvi wa hili wahini kabla #Ngwini# hawajachafua uzi huu kwani wao kila kitu ni povu tuu.

Direct to the point;
Tumekuwa tukiaminishwa yakuwa mwaka una siku 365 na robo, swali ni je katika hizi siku tatu zilizo salia yaani tar 29, 30, 31 ile robo ilishapita au ipo kwenye hizo siku zilizobakia na kama ndio au lah hiyo robo inakuwaje kuwaje?.
 
Ile robo ni Magumashi
Labda nijitahidi kukueleza navyojua.

Siku ina masaa 24. Hivyo masaa 24 ni siku moja hayo masaa ni nasibu/arbitrary tu.

Kipimo sahihi cha hiyo siku yenye masaa 24 ni mzunguko wa dunia katika mhimili wake ambao unachukua takribani masaa 24 ndiyo tunapata one day..

a year: hapa tunapima mwaka Kwa dunia kujizungusha katika jua. Jua likimaliza mzunguko wake kutoka point X to point ileile ya mwanzo X ndipo tunapata mwaka mmoja.

Hivyo hizo siku nazo ni nasibu pia, ule muda Dunia inapomaliza mzunguko wake ndipo mwaka huhesabika hizo siku ziweke kwenye masaa utaelewa somo vizuri usimeze siku itahesabika pale tu itakapofika saa 00.00. Na kuna mwaka mfupi na mrefu[hili naamini unalijua].

Kila baada ya miaka 4 hizo siku 0.75 hujakamilisha na huwezi ukaona. Au ulitaka mzunguko ukiishia saa Saba basi giza liingie muda huo hakafu kukuche muda huo huo?
 
Siku 28, 29, 30, 31... kwanini mna base katika siku 28 na 29? kwanni 30 na 31 mnaziacha... labda kama siku zingekuwa 30 au 31 alafu hizi 28 na 29 ndio zinakuja kuleta hayo mabadiliko...

Pia huu ugunduzi wa kalenda ulifanyika miaka ya karibuni hapa... je kabla ya hapo walikuwa wana ishi kwa kipimo gani cha kung'amua ukubwa wa mwaka siku na miezi? au ilikuwa kama jera usiku na mchana?
 
Uliza nami ntajaribu kukuelewesha ninavyojua
 
Uliza nami ntajaribu kukuelewesha ninavyojua
Siku 28, 29, 30, 31... kwanini mna base katika siku 28 na 29? kwanni 30 na 31 mnaziacha... labda kama siku zingekuwa 30 au 31 alafu hizi 28 na 29 ndio zinakuja kuleta hayo mabadiliko...
Pia huu ugunduzi wa kalenda ulifanyika miaka ya karibuni hapa... je kabla ya hapo walikuwa wana ishi kwa kipimo gani cha kung'amua ukubwa wa mwaka siku na miezi? au ilikuwa kama jera usiku na mchana?
 
Kabla ya kalenda watu walitumia sana elimu ya nyota,hasa hasa the Ancient greeks who were the first true astronomers.zaidi ya hilo tuna vitu vinaitwa constellations navyo vilitumiwa sana!!!Mambo haya ya kugawa mwaka yamekuja baada ya wa Egypt kugundua kalenda na kuugawanya mwaka katika miezi 12
 

Kipimo sahihi na kinachotumiwa ni Dunia inapokamilisha Mzunguko kwenye Jua.

Hizi calenda ni unasibisho tu ndiyo maana zamani kila jamii ilikuwa na namna ya kuupima/kuuweka muda wake muda ulipimwa kwa matukio, nyota, mwezi, Egyptians walikuwa na calenda yao baadae, Wagiriki walikuwa na calenda yao, Roman pia walikuwa nayo n.k

Sema Gregorian calendar ndiyo ilikuja kuaminika zaidi kwa kuhusianisha uhesabuji siku na mfumo jua. Na ndiyo inayotumika kwa wengi duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…