MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Winga machachari wa ujerumani na klabu ya Manchester City Leroy Sane amewashangaza wengi baada ya kuitaja Tanzania alipofanya mazungumzo na jarida la michezo la Kicker sportmagazin.
Sane pamoja na mambo mengine mengi aliyoongea na gazeti hilo alitaja maisha aliyoishi Tanzania wakati baba yake akiifua timu ya Zanzibar,Leroy alidai wakati wa likizo alikuwa akija Dar es Salaam kumtembelea baba yake Suleiman Sane(aliifundisha Zanzibar miaka ya kati ya 2000 ) na walikuwa wakifanya mazoezi pamoja katika kiwanja cha Bandari TMK na amedai anatamani sana kurudi Tanzania kama kocha au kufungua shule ya mpira akistaafu soka.
Kila la kheri kijana