Hallo ni jambo la hatari sana. Mimi nimefanyiwa operation ya macho juzi nimepona. Sasa hivi nawaheshimu sana ma doctor wa macho. Tatizo ilikuwa jicho moja lilianza kupata giza.
Tatizo la macho ni kwamba hata kama unaona kidogo ile kukadiria umbali wa kitu inachangamoto na katika kundesha hayatakiwi haya makosa aidha utagonga au utagongwa. Nakumbuka kuvuka barabara ilibidi niwe najipanga sana. Tatizo sio kuona, ila kukadiria eneo au kitu kiwe kiko palepale au kinatembea utachemsha tu.
Matatizo mengine ya macho ni kwamba taa za gari za kawaida kwako unaona kama "Full".
Labda inategemea na shida yenyewe na uzoefu wa mwenye tatizo la kacho.