Leseni ya biashara ni wakati gani.

Leseni ya biashara ni wakati gani.

chardboy77

Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
53
Reaction score
5
samahani wadau, mimi nahitaji kufanya biashara za e_money kijijini kwetu manake wananchi wanapata shida huku. Nauliza leseni ya biashara huwa inakatwa baada ya kuanzisha biashara au kabla? Na proces zake ni aje?
 
kabla haujaanza biashara hatua ya kwanza nenda wilayani kachukue fomu za uombaji wa lenseni uijaze kisha peleka wilayanii watakupangia utaratibu wa installment ya biashara yako
samahani wadau, mimi nahitaji kufanya biashara za e_money kijijini kwetu manake wananchi wanapata shida huku. Nauliza leseni ya biashara huwa inakatwa baada ya kuanzisha biashara au kabla? Na proces zake ni aje?
 
Kwanza uwe na TIN inapatikana TRA kisha nenda kwa afisa biashara ukiwa na kitambulisho na uthibitisho wa eneo la biashara. Utapewa fomu ukalipie bank na ada ndogo kabisa ni Tsh 40,000(saloon)
 
nashukuru, sasa uthibitisho wa eneo la biashara ndo upi?
 
mkataba wa kupanga eneo la biashara,au risiti ya malipo ya jengo kama unamiliki hapo unapofanyia biashara,au kama hapajapimwa na hapalipiwi jengo barua ya mtendaji kuthibitisha kuwa unamiliki nyumba hiyo
 
Back
Top Bottom