Hii mada inaonesha kweli haijajitosheleza hata kama unataka kuita fununu / nyepesi nk.
Kama Mengi aliomba leseni, basi aliomba kivyake kama wanavyoomba wengine ikiwemo vodacom, Mobitel, Tritel, Celtel nk. Sasa unaposema kuwa Mengi aliomba akanyimwa akapewa Vodacom, haileti maana yoyote zaidi ya kuwa maelezo yako hayajakamilika.
Inawezekana kuwa aliomba leseni kabla ya Vodacom, lakini kama hakukidhi haja au masharti yaliyomo katika maombi sidhani kama ageliweza kupewa tu just because ni Mengi.
Kumbuka katika sakata la Mengi vs Masilingi:
Mengi aliomba kuuziwa Kilimanjaro Hotel lakini hakuwa ametimiza masharti ya maombi yale kwa hiyo hakuweza kununua Hoteli ile ( Japokuwa alikuwa anataka kununua kama middleman).
Kumbuka katika sakata la Mengi vs Mama Munyagi (DG wa TCAA):
Mengi akiwa backed na 'wajanja wa mjini' Musiba na Kaunda na kwa kutumia vyombo vyake vya Habari, alimshutumu hadharani Mama Munyagi kuwa anamuonea hataki kumpa leseni ya kurusha Air Bus iliyoletwa kwa ajili ya Kampuni ya Ndege ya Africa One.
Msimamo wa Mama Munyagi usiotetereka hatimaye ulimletea aibu Mzee mzima Mengi na hata mwishowe kuwatupia lawama Musiba na Kaunda na hapo ndiyo ukawa mwanzo na mwisho wa Africa One.
Kwa hiyo sidhani kama kunajambo lolote lililomzuia au linalomzuia Mengi kusajili kampuni ya simu za mikononi