Wakuu,
Nimekuwa nikifuatilia suala la leseni ya udereva tangu April hadi leo sijapata. Naambiwa Hazitolewi, kuna ukaguzi sijui wa vyeti.
Naomba kujua kama ni kweli zoezi limesimamishwa au la. Kama halijasimamishwa, naomba kujua nitumie mbinu gani kuipata kwa haraka.
Nimekuwa nikifuatilia suala la leseni ya udereva tangu April hadi leo sijapata. Naambiwa Hazitolewi, kuna ukaguzi sijui wa vyeti.
Naomba kujua kama ni kweli zoezi limesimamishwa au la. Kama halijasimamishwa, naomba kujua nitumie mbinu gani kuipata kwa haraka.
- Tunachokijua
- Kumekuwa na uvumi unaenea ukidai kuwa Leseni za Udereva nchini Tanzania zimesimamishwa kutolewa tangu Mwezi Aprili, 2023. Taarifa hizo zinadokeza kuwa Mamlaka ya Utoaji wa Leseni imesimamisha zoezi hilo mpaka wahusika watakapokuwa na vyeti.
Baada ya kusambaa kwa madai haya, JamiiForums imemtafuta Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Polisi Usalama Barabarani Tanzania, Ramadhani Ng'azi ili kupata ufafanuzi wa kinachoendelea.
Katika Maelezo yake, Ng’azi amethibitisha kuwa kuwa zoezi halijasitishwa. Amesema;
"Zoezi halijasitishwa linaendelea na hata leo nipo kwenye ofisi mchakato unaendelea. Kilichotokea ni kuwa Machi 2023 Dawati la Leseni lilivunjwa kutokana na leseni kutolewa kiholela na kuwapa watu ambao hawakuwa na sifa ya udereva"
Ameendelea kusema "Wakapatikana vijana waadilifu wachapakazi, wazalendo wakakabidhiwa majukumu na mchakato ukaendelea kama kawaida"
Katika hatua nyingine, Ng'azi amebainisha kuwa kinachofanyika sasa ni uhakiki wa Leseni hadi Julai 31, 2023 ambapo dereva ambaye hana sifa tunamfutia madaraja, baada ya hapo madereva ambao hawajahakikiwa kwa hiyari watakamatwa.
Awali, baadhi ya wadau walilalamikia pia uwepo wa changamoto kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)kwenye kushughulikia malipo ya leseni. Akizungumza na JamiiForums, Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa kodi (TRA), Richard Kayombo anasema zoezi halijasitishwa kilichofanyika ni maboresho ya upatikanaji wa Leseni za Madereva.
"Taratibu za utoaji Leseni zipo chini ya Jeshi la Polisi, wao ndio kwa asilimia kubwa wanasimamia kabla ya kuja kukamilika kwetu, hivyo wanaweza kuwa na majibu sahihi lakini kwa ufupi yamefanyika maboresho na sio kusitisha utoaji Leseni"
Utaratibu wa Kuomba leseni ya udereva kwa mara ya kwanza
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mhusika anayetaka kuomba leseni ya udereva kwa mara ya kwanza hupaswa kufuata vigezo 7 kama ilivyoainishwa hapa chini;
- Uwe umehudhuria mafunzo katika Chuo chochote kinachofahamika na kupewa cheti
- Uwe na umri zaidi ya miaka 18 kwa ajili ya gari na umri wa miaka 16 na kuendelea kwa ajili ya pikipiki
- Uwe na leseni ya kujifunzia/ya muda ya udereva
- Uwe umelipa ada ya kufanyiwa majaribio - GRR
- Uwe na cheti cha kupimwa macho
- Uwe umepeleka maombi kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani kwa ajili ya kufanyiwa majaribio
- Uende kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani ukiwa na gari kwa ajili ya kufanyia majaribio