Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

Nimepata uhalisia wa mambo mengi kuwasikia wazanzibar UKWELI HAUJIFICHI NAHUO NI UKWELI KUTOKA KWAO

1. CCM INAWAPELEKA KULE AMBAKO HAWAKUTAKI (VIONGOZI WAO KUCHAGULIWA TANZANIA BARA)
MFANO NA NIKWELI RAISI LAZMA APELEKWE DODOMA WANASEMA HAWALITAKI NA HILI NI KWELI WANASEMA LAZMA IKIWA CCM AU CHAMA CHOCHOTE KIONGOZI LAZMA ITOSHE ACHAGULIWE KULE KULE ZANZIBAR

2. SUALA LA KATIBA MPYA LIMEHUSISHA KUTOKUPENDEKEZA MUUNGANO UWEPO AU USIWEPO UKWELI WENGI WANGEKATAA LABDA CCM KULAZIMISHA SABABU KIAKILI NI KWELI UMEUNGANA NA NANI AMBAE HATAKI KUJITAMBULISHA. NDIO WAKAJA AFADHALI KUSEMA SEREKALI 3 ILI IMTAMBUE ALOUNGANA NAE BILA KUJIFICHA

3. ZANZIBAR NI KISIWA HIVO HUWEZI KUFANANISHA NA NCHI KAMA TANZANIA AMBAYO UCHUMI WA TANZANIA UNATEGEMEA RASILI MALI NYINGI ZA ARDHI YAKE TAFAUTI NA ZANZIBAR AMBAYO UCHUMI HAUTEGEMEWI SANA NA ARDHI ILA NI UCHUMI WA KUTENGENEZA HUDUMA (SRVICE ORIENTED ECONOMY) HII NI KWELI WANASEMA SEREKALI YA MUUNGANO AMBAYO NI YA TANGANYIKA HAIJAFANYA MRADI HATA MMOJA KWA MASUALA KUENDELEZA UCHUMI WA ZANZIBAR KUPITIA HUDUMA BALI HUTAKA KUTUMIA ARDHI PEKEE IWE NI KIGEZO CHA UCHUMI

MFANO: UCHUMI WA HUDUMA IWE KAMA BAHARI KUTUMIKA KUZALISHA NYENZO MBALIMBALI ZA UCHUMI WAO KUTOA HUDUMA PAMOJA NA UVUVI

HAPAJAKUA NA UHUSIKA WA MUUNGANO: WANASEMA KWAKUA SEREKALI YA MUUNGANO IMEBEBA UHUSIKA WA KUPEWA HABARI JUU YA KILA JAMBO NA KUTOA ,MAAMUZI HIVO MAAMUZI TAKRIBANI YOTE HUPUUZWA KWA KUA HUENDA KINYUME NA UCHUMI WA RASILI MALI YA KUPITIA ARDHI .

NAMALIZIA KUSEMA TIZAMA LINK HII

https://www.youtube.com/watch?v=AFuy14au6Ws
 
hatupingi muungano tunapinga tanganyika kuvaa koti la muungano

Muongo!

Nafasi si hii sasa mbona wote mnayakataa maneno yenu wenyewe!. Nafasi hii ikipita tusiwasikie mnaleta choko choko yoyote tena, tumechoka. Hatufanyi shughuli zetu ni kelele tu, tunaonewa, tunaonewa. Nafasi mmepata ya kutoa malalamiko yenu, mnageuka kuwa hamjasema.

Nasema nafasi ikipita mnyamaze kimya, tusiwasikie tena, tumechoka kelele!
 
ss tunaendelea kuimba:
"umelala huooo umelala huooo umelala huo mtarimbo umelala dorooo..."

"wache ulale dorooo"
 
Tukiamua kufuata sheria, taratibu na kanuni, muungano ni kwa bara tuu, kwa Zanzibar hauna legitimacy, hivyo kuuvunja from that side ni haki yao.

Naunga mkono hoja!.

Pasco.
Baada ya somo kutoka Uingereza, Zanzibar sasa milango i wazi!.

Pasco
 
Katika dili liliobaki ambalo wabara hatulipendi na wa ZNZ hawalitaki ni muungano. Lakini hatujawahi pewa fursa ya wazi kulijadili na kulifanyia maamuzi.
 
Baada ya somo kutoka Uingereza, Zanzibar sasa milango i wazi!.

Pasco

MILANGO HAIKO WAZI KATIKA HALI YA KUVAMIWA NA VITA VYA KIDINI CHINI YA MZIMU WA KIKATOLIKI WA NYERERE

Desemba 1993

MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.

Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:

Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.

Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.

Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.

Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.

Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge; wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili. Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu. Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka). Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.

Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:

Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.

Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.

Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.

Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.

Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!

Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.
 
"kontakinte, post: 9639939, member: 148449"]Nimepata uhalisia wa mambo mengi kuwasikia wazanzibar UKWELI HAUJIFICHI NAHUO NI UKWELI KUTOKA KWAO
Je, wanazungumza ukweli hata ule mchungu kwao?
1. CCM INAWAPELEKA KULE AMBAKO HAWAKUTAKI (VIONGOZI WAO KUCHAGULIWA TANZANIA BARA)
MFANO NA NIKWELI RAISI LAZMA APELEKWE DODOMA WANASEMA HAWALITAKI NA HILI NI KWELI WANASEMA LAZMA IKIWA CCM AU CHAMA CHOCHOTE KIONGOZI LAZMA ITOSHE ACHAGULIWE KULE KULE ZANZIBAR
Kama hawataki Rais achaguliwe Dodoma, wanapaswa kukataa pesa kutoka hazina Dar.
2. SUALA LA KATIBA MPYA LIMEHUSISHA KUTOKUPENDEKEZA MUUNGANO UWEPO AU USIWEPO UKWELI WENGI WANGEKATAA LABDA CCM KULAZIMISHA SABABU KIAKILI NI KWELI UMEUNGANA NA NANI AMBAE HATAKI KUJITAMBULISHA. NDIO WAKAJA AFADHALI KUSEMA SEREKALI 3 ILI IMTAMBUE ALOUNGANA NAE BILA KUJIFICHA
Pale Dodoma walikuwepo wazanzibar tena walioungana na CCM. Unaposema wengi, ni wapi hao?

3. ZANZIBAR NI KISIWA HIVO HUWEZI KUFANANISHA NA NCHI KAMA TANZANIA AMBAYO UCHUMI WA TANZANIA UNATEGEMEA RASILI MALI NYINGI ZA ARDHI YAKE TAFAUTI NA ZANZIBAR AMBAYO UCHUMI HAUTEGEMEWI SANA NA ARDHI ILA NI UCHUMI WA KUTENGENEZA HUDUMA (SRVICE ORIENTED ECONOMY) HII NI KWELI WANASEMA SEREKALI YA MUUNGANO AMBAYO NI YA TANGANYIKA HAIJAFANYA MRADI HATA MMOJA KWA MASUALA KUENDELEZA UCHUMI WA ZANZIBAR KUPITIA HUDUMA BALI HUTAKA KUTUMIA ARDHI PEKEE IWE NI KIGEZO CHA UCHUMI
Mradi ni ule wa nusu ya wazanzibar kuishi bara raha mstarehe. Unataka upi mkubwa zaidi ya huo?

MFANO: UCHUMI WA HUDUMA IWE KAMA BAHARI KUTUMIKA KUZALISHA NYENZO MBALIMBALI ZA UCHUMI WAO KUTOA HUDUMA PAMOJA NA UVUVI

HAPAJAKUA NA UHUSIKA WA MUUNGANO: WANASEMA KWAKUA SEREKALI YA MUUNGANO IMEBEBA UHUSIKA WA KUPEWA HABARI JUU YA KILA JAMBO NA KUTOA ,MAAMUZI HIVO MAAMUZI TAKRIBANI YOTE HUPUUZWA KWA KUA HUENDA KINYUME NA UCHUMI WA RASILI MALI YA KUPITIA ARDHI .
Na kwakuwa serikali ya muungano imebeba mzigo wa muungano na ikiwemo znz, ina haki ya kumua nini hasa ni muhimu na kwa wakati gani
 
Kuelekea kumbukumbu ya Mapinduzi hapo kesho, hakuna ubaya kutafakari, should we let them go? .

Paskali
 
Kwa wasiojua ukweli wa mambo, msingi mkuu wa muungano ni dhima ya Nyerere na Karume in good faith!.

Baada ya dhima ikafuatia kitendo cha kuungana rasmi kwa kuchanganya udogo na kusaini zile hati za muungano.

Baada ya hapo muunngano huo uliridhiwa bara tuu (ratified) kwa bunge la Tanganyika kuupitisha mkataba huo uliokuwa na mambo 11 hivyo kupata nguvu za kisheria!.

Zanzibar nao walitakiwa kuuridhia mkataba huo wa muungano kwa kuuratify lakini jambo hili halikufanyika!. Hivyo wanasheria wangeweza kabisa kuishitaki Tanzania kwa kuipora mamlaka Zanzibar na kuikalia kimabavu miaka yote hiyo!.

Kufuatia kukosekana kwa uhalali wa kisheria wa muungano kule Zanzibar, hivyo Wanzanzibar wako huru kujitoa kwenye muungano kwa amani kabisa kwa kung'ang'ana kuwa sheria, taratibu na kanuni, hazikufuatwa!.

Maadam Wanzanzibari wanacholilia ni haki na uhuru wao, nawaombeni tuwateende haki kwa kuwapatia wanachotaka.

Naiunga kauli ya Mzee Mwanakijiji kwa asilimia 100%, "Let them go!."
Nawatakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano.
Paskali
 
20210426_173416.jpg
 
MMKJJ,
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, hoja yoyote ya kuuvunja muungano ni uhaini!.

Angalieni jf tusije nyooshewa vidole tuu wachochezi!.

Tukiamua kufuata sheria, taratibu na kanuni, muungano ni kwa bara tuu, kwa Zanzibar hauna legitimacy, hivyo kuuvunja from that side ni haki yao.

Naunga mkono hoja!.

Paskali
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Back
Top Bottom