Kwanza nashukuru wote kwa kuchangia.
Swali kwenu, ikiwa kila kitu tulichonacho Serikali ikishindwa kukiendesha au kusimamia utendaji, inakimbilia kutafuta Wawekezaji au Wabia, kwa nini basi tusitafute Wawekezaji au Wabia kutoka nje ya nchi ili waongoze nchi yetu?
Tuna Katiba, Sheria na kanunu elfu zinazoongozwa na miongozo, itikadi, falsafa na ilaniza Chama/Vyama. Lakini kila siku tunashindwa kazi. tunashindwa kuwa wabunifu, wafanisi, wadadisi, wachapa kazi, waadilifu, wawajibikaji na kuishiwa kuwa wazembe, wahujumu, mafisadi, wavivu, wategaji na omba omba.
Ikiwa Serikali ambayo ndiyo inapaswa kutoa mwongozo na kuhamasisha uzalishaji mali inainua mikono juu na kusema tunatafuta wabia na wawekezaji kuokoa uzalishaji mali wa mashirika, viwanda, biashara na hata sasa kwenye kilimo, kutokana na kushindwa kuwa wabunifu na wenye kutumia juhudi na maarifa kuleta maendeleo ya kweli, je kuna faida gani kuwa ni Serikali ya watu wale wale ambao hata akija Rais mpya, hakuna litakalo badilijka?
Nyerere alikaa madarakani miaka 23. Mwinyi, Mkapa na Kikwete wamekalia kiti hicho hicho kwa miaka karibu 23. Katika miaka hiyo 46, Kikwete, Wasira, Msekwa, Malecela, Salim, Chenge, Sitta, Mzindakaya na wengine wengi, wameendelea kuwa viongozi (na wabunge) ndani ya Serikali na Chama na hata kuwa na sauti kubwa.
Sasa kama kwa miaka 46, wameshindwa kuwa na msukumo wa kweli wa kuleta maendeleo kwa Taifa na kupiga vita Ujinga, Maradhi na Umasikini na sasa kila mtu anakimbilia kutafuta "Panadol" ya kuuza kila kitu kwa Wageni wabia na wawekezaji si kauli jificho kuwa hatuwezi kujiongoza?
If that is the case, why not privatize the damn government? Let Mkoloni or Mwekezaji aje tuanze kupeta.
Interestingly, kila mahali alipo Mwekezaji na Mbia, kuna nidhamu ya hali ya juu, watu wanachapa kazi kwa bidii, ufanisi na ushindani. Inakuwaje sisi wenyewe tunashindwa kujitawala?
Je ni kosa letu wananchi au ni wale tunaowachagua na kuwapa dhamana ya kutuongoza wamekosa mwamko na kushindwa kutumia ipaswavyo sheria, kanuni na mipango ili kuhakikisha kuwa ama nidhamu ya kazi ina kuwa ni hiari na si mambo ya nidhamu ya woga, juhudi za maendeleo zinakuwa ni nia thabiti ya kila Mtanzania ili kuondokana na maadui watatu na si kujaza mifuko na hazina za wawekezaji?
Ni mpaka lini tutaendelea kusuasua katika hii safari ya kutokujijua? Hata tukimpa ndugu yangu Kitila au Zitto urais, je tunaamini tutabadilika na kuwa wachapakazi na watendaji mahiri, wafanisi, bunifu, adilifu na wawajibikaji? au tutadumisha Mizengwe kama kawaida?
Please someone go and search for Sir Richard Turnbull, lets privatise the damn country! and we can enjoy masufuria ya Misri!