kosa nililolifanya mimi ilikuwa ni kuwashirikisha wanafamilia na marafiki ambao wote ni waajiriwa na hakuna aliye na hata kabiashara ka duka. Mkuu tangulia tupo njia moja.
nilima mpunga kijijini baada ya kukoboa nilipata gunia zaidi ya 50 za mchele niliingiza around ---- 12.2m
niliilima mahindi na kuyasaga nilipata gunia kama 130 za sembe 900 per kg nilipata zaidi ya --------10m
ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, nauza lita 1000-1200/= na kila siku napata lita si chini ya 75 ---- naingiza 2.5m kila mwezi--- kwa mwaka ng'ombe wananipa ---27m
ufugaji wa nguruwe kwasasa ninao kama 80 na 8 wana mimba----- kila mwaka natarajia kuuza 150--- roughly let say nitapata around 40m
nalima maharagwe, njugu, matikiti kiasi, maembe nk nayo yanaingiza fedha nzuri sana japo sijui mahesabu yake halisi
Majumuisho
total = 10m+10m+27m+40m= 87mil
ukitoa operating costs profit will be around let say 45m kwa makisio ya chini kabisa na hapa ni baada ya kuibiwa sana mazao ya kilimo na mifugo na hii nguvukazi yangu ambayo haina uaminifu hata kidogo yaani kila nikibadili vijana wa kazi wanakuwa na uadilifu kwa miezi 3 ya mwanzo baada ya hapo matatizo ni yaleyale wizi kwa kwenda mbelee.. watu wameoa, wamejenga kwa jasho langu.
Mkuu hebu angalia hapa maziwa nispokuwepo yanapatikana lita 50-70 nikiwepo mwenyewe na kusimamia ukamuaji zinapatikana lita 90 mpaka 100. Mchele nikiacha gunia 10 nikienda mjini na kurudi kijijini nakuta zimebaki gunia 7 nikiuliza sipati majibu.. inaniuma sana sana.. nataka kwenda kusimamia kazi zangu mwenyewe[/QUOTE]
mkuu hapo pa bluu umenitonesha kidonda,yaani watu si waaminifu mkuu mim wafanyakazi waliniibia sana mwishowe nikaamua kuajiri ndugu zangu toka kijijini,walipozoea tu mazingira walinitenda sana roho inauma sana lkn sina jinsi.Heri wewe umeamua kwenda kusimamia mwenyewe,mim natamani nikasimamie mwenyewe sbb simuamin tena mtu lakini kwa sasa haiwezekani.