Letter of credit: Faida na hasara zake

Asante sana..sasa nimeelewa vema!!
 
malenga wetu asante kwa mada nzuri.

Inavyoonekana wewe unauelewa mpana tu kuhusu L/Cs ingawa ulipoanzisha uzi umeonyesha kutaka kujuzwa faida na hasara zake. Nashauri umwage maujuzi yote hapa wana JF tufaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kiuhalisia hii ndio bidhaa kuu inayoniweka mjini ... naamini naweza kujibu maswali mengi kuhusu ''LC'' na msaada wa kitaalamu pia (Karibu PM ama +255 22 216 1498).

Ningependa kujibu maswali yako katika hali ya kawaida kabisa (si kitaalamu sana) ili wengi tushiriki katika kile nikijuacho na ninachokifanya hapa kwenye desk langu, sitaenda deep sana ...

1. Letter of Credit inavyofanyaje kazi

Kwa kawaida LC inaanza baada ya muuzaji na mnunuaji wanapokuwa tayari wameingia kwenye makubaliano ya kufanya biashara na pia kukubaliana kutumia njia hii (LC) ... coz LC ni mojawapo tu ya njia za kufanya malipo katika biashara za kimataifa. Njia nyingine ni Advance Payment na Open Account ambazo kama ilivyo LC zina faida na hasara zake (LC ndio njia salama zaidi kupita zote na ndio maana ni ghali zaidi pia coz all the risk is going to taken by the bank) ....

Baada ya makubaliano, then mnunuzi ndiye anayetakiwa kwenda kwenye Bank yake na kuulizia bidhaa hii ambayo kwa Bank ''Iliyo karibu yako'' waweza kutana nami. Kwa kifupi jinsi inavyofanya kazi ni kwamba mnunuzi kwa kutumia akaunti uliyonayo kwenye bank husika, utatujazia LC application form ambapo utatupa taarifa muhimu za kwako binafsi, supplier wako na bank yake e.t.c pamoja na profoma invoice ...

Then bank yako say (NMB Plc) itawasiliana na Bank ya supplier wako say (Bank of China) then wao watawasiliana na supplier wazo kuhusu document zinazohitajika, ubora na wingi wa bidhaa unaohitajika na document za umiliki ... ambazo endapo zitawasilishwa THEN atapata malipo yake.



2. Faida na hasara zake

Faida ni nyingi sana zikiwemo, usalama(security), uhakika wa kupata bidhaa katika kiwango na ubora unaohuitaji na refund endapo mambo hayataenda sawa. Kwa kutumia LC uwezekano wa kutapeliwa haupo kwani muamala wenu unahusisha Bank na Bank na si mtu na mtu ama mtu na Bank ...

HASARA ni chache sana zikiwemo, gharama .. I mean Bank zinachaji ku-offer LC (0.56% ya Invoice value kwa 3 months) min. USD 223, mahitaji/masharti pia yaweza kuwa magumu kwa wengine i.e Lazima uwe na Bank akaunti, lazima utimize masharti yote mliyokubaliana bila kukosa, pia pindi unapoindia makubaliano huwezi kuyavunja bila kukubaliana na pande mwenza.

Pia hasara nyingine, ni kwmba lazima uwe na fedha za kutosha kufanya muamala pamoja na charges vinginevyo bank zinaweza kukupa ''MKOPO'' ambapo sote tunajua masharti, faida na hasara za mkopo.

3. Pia risk involved kwenye matumizi ya letter of credit.

As per 2. above ...



(kwa maswali na maongezi yakinifu waweza nicheki hapa +225 22 216 1498 (JINA: munisijo)
 
Jamii ni sehemu nzuri ambapo unapata weredi wa kutosha maana mimi nilikuwa nasikia sana lc but nilikuwa sijui maana yake..thankx all wadau kwa kutuelimisha
 
Asante sana..sasa nimeelewa vema!!

Niliwahi kuitumia like 3 yrs ago through CRDB. Ni nzuri unapokuwa na wasiwasi kuhusu kutapeliwa mzigo usije. Unatakiwa kufungua foreign currency account (escrow account) ndo unaweka hizo hela, zinakuwa mikononi mwa bank. Kimsingi bank ndo inakuwa guarantor wa kuhakikisha mzigo umekuja na kuhakikisha supplier amelipwa hela yake.

Hata docs za mzigo (bill of landing, Invoice) zitatumwa benki, we utaenda kupokelea benki. Wakishakukabidhi hizo docs the deal is over, kifuatacho wanatarelease hela kwa supplier regardless mzingo utafika ktk ubora wake au la.

Wao wanathibitisha ubora wa mzigo kwa kukagua specifications ktk docs baaasi. Kimsingi watarelease hela kabla hata mzigo haujafika, so ufike usifike si suala lao tena, hilo ni suala la shipping line pamoja na insurance kama kuna upotevu wa mzigo, uharibifu etc.

Nilitumiaga once, na sijaona umuhimu wake tena kwa sababu ya hizi mambo za paypal na nini, coz ni more or less the same. Tena hawa paypal na nduguze wanaenda mbali zaidi kukukagulia mzigo. Nitaitumia tu pale ambako hakuna huduma ya paypal n.k
 
mito asante kwa maelezo. Ila sijakusoma hapo unaposema kwamba bank watarelease pesa kwenda kwa supplier regardless mzigo utafika au hautafika. Pia haijalishi kama mzigo utafika ktk ubora wake ama la. Mbona inapoteza maana? au mimi ndo sijakuelewa?
 
Last edited by a moderator:
mito asante kwa maelezo. Ila sijakusoma hapo unaposema kwamba bank watarelease pesa kwenda kwa supplier regardless mzigo utafika au hautafika. Pia haijalishi kama mzigo utafika ktk ubora wake ama la. Mbona inapoteza maana? au mimi ndo sijakuelewa?

Ulivyoelewa ndo hivyo hivyo nilivyomaanisha mkuu. Ndo maana nimesema ipo kwa ajili ya kuzuia utapeli zaidi. Manake wao wanadili na usahihi wa documents. So mfano kama ni gari, wao wataangalia specifications ulizowapa halafu wanalinganisha na zile za kwenye bills of landing, invoice etc. Wakikuta ziko sawa, basi wanakukabidhi docs zako uendelee na mchakato wako wa kutoa mzigo bandarini, wao wanarelease pesa kwa supplier.

Ila nikutoe wasiwasi, bills of landing ni uhakika kuwa mzigo utafika na uthibitisho kuwa mzigo umeishapakiwa melini, jamaa wa shipping line hawanaga ubabaishaji. Wasiwasi ni kwenye ubora wa mzigo wako baasi.

Kwa kuzingatia ishu ya ubora ndo maana nimesema mi niliwatumiaga letter of credit mara moja tu nikaachana nao. Siku hizi natumia akina Paypal na jamii zake kwani wao wanaenda zaidi hadi kukagua ubora wa mzigo.
 
Kwa ufahamu wangu, ni kuwa ukaguzi wa mzigo anafanya muagizaji, akiridhika anaweza toa ridhaa kwa bank kuendelea na malipo ya mzigo.
 
na pia letter of credit zinawekwa terms na conditions, zikiwa sawa malipo yanafanyika kwenda kwa bank ya muuzaji bidhaa, wewe kama mnunuzi unaweza weka conditions kwa bank yako isitoe malipo mpaka labda ufanye ukaguzi wa mzigo wako, na ni lazima ikubaliwe na muuzaji pia.
Ila ni njia moja iliyo salama, kama parties zote zitakuwa zimeelewana katika kufanya hiyo biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…