Niliwahi kuitumia like 3 yrs ago through CRDB. Ni nzuri unapokuwa na wasiwasi kuhusu kutapeliwa mzigo usije. Unatakiwa kufungua foreign currency account (escrow account) ndo unaweka hizo hela, zinakuwa mikononi mwa bank. Kimsingi bank ndo inakuwa guarantor wa kuhakikisha mzigo umekuja na kuhakikisha supplier amelipwa hela yake.
Hata docs za mzigo (bill of landing, Invoice) zitatumwa benki, we utaenda kupokelea benki. Wakishakukabidhi hizo docs the deal is over, kifuatacho wanatarelease hela kwa supplier regardless mzingo utafika ktk ubora wake au la.
Wao wanathibitisha ubora wa mzigo kwa kukagua specifications ktk docs baaasi. Kimsingi watarelease hela kabla hata mzigo haujafika, so ufike usifike si suala lao tena, hilo ni suala la shipping line pamoja na insurance kama kuna upotevu wa mzigo, uharibifu etc.
Nilitumiaga once, na sijaona umuhimu wake tena kwa sababu ya hizi mambo za paypal na nini, coz ni more or less the same. Tena hawa paypal na nduguze wanaenda mbali zaidi kukukagulia mzigo. Nitaitumia tu pale ambako hakuna huduma ya paypal n.k