yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,662
- 3,715
Ikinyesha mvua kubwa haisombi huo udongo mkuu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona nimeshakosea. Napaswa kupasahau kidogo ili nifanye Mambo mengine. Au kuamua alternative nyingine ya kupauza kabisa nikatafute kwingineMkuu kama ni nyumba kubwa kwa aina ya viwanja hivyo basi amini kwamba utazika nyumba nyingine kwenye msingi tu.
Hapo mbinu nzuri ilikuwa ni kuitafuta level kwa kunyanyua msingi mrefu (kutoka kwenye ardhi halisia uliyoikuta) upande wenye slope mpaka ulingane na ule upande ulioko kwenye muinuko, baada ya hapo yale mashimo marefu yatakayopatikana kwenye partition za msingi ndo ujaze vifusi utakavyo mpaka palingane.
Lakini pia kifusi utakachojaza kwenye hizo partition za msingi kakikisha zinashindiliwa vizuri kabida either kwa kuziacha muda fulani au kama upo vizuri mfukoni na una haraka za kuanza ujemzi, jaza maji mengi kabisa kwenye hizo partition ili udogo utitie vizuri na ujishindilie kisha leta comprassor shindilia tena.
Kama msingi ni wa tofali (nashauri ziwe nchi sita), kabla haujaanza kunyanyua boma basi funga beam na umwage zege, weka PVC halafu anza kupandisha boma sasa.
Kujenge kwenye viwanja vyenye miteremko ni gharama sana ikiwa utataka kujenga nyumba yenye standard, kwakua gharama za kuset msingi tu zinaweza kulingana au kuzudi kabisa gharama za kunyanyua boma kwenye kiwanja ambacho ni tambarare.
NB: Msingi wako upigwe maji ya kutosha na ratio ya cement isiwe ya kinyemela (ndoo 12 ndogo za mchanga kwa mfuko mmoja wa cement)
Naona nishachemsha. Inabid nijipe muda wa kutafakar nione Cha kufanya Kama Ni kuuza au kuvumilia huku nikifanya shughul nyingineMkuu kwa swala la muda sio kipaumbele sana...BUT hapo lazima uache for at least miaka 3+ ili ardhi ikae sawa kidogo,,,na hapa ni kwa ujenzi wa nyumba ndogo tu ya kuishi...
Kama uko speed Hakikisha msingi wako unaanzia kwenye Ardhi asilia....
Ukifanikisha hilo anza kujenga...Otherwise usipofika chini msingi utaelea..
Nitakuja na picha
Naona nishachemsha. Inabid nijipe muda wa kutafakar nione Cha kufanya Kama Ni kuuza au kuvumilia huku nikifanya shughul nyingine
Picha haifunguki. Ila Asante kwa maelezoDaah. Umekosa sana mkuu. Hizo gharama za levelling bora ungeingia gharama kunyanyua msingi tu. Nimefanya kama ulivyofanya wewe ila ni baada ya kujenga nyumba ndogo na kuacha matolea. Kwa Sasa imepita miaka mitatu ila bado Sina Imani ya kuvuta hii nyumba. Nawaza kupiga underground tu
Ukiangalia huku nyuma niliacha matoleo lengo ni kuja kuweka sebule, dining, Jiko na vyoo ila bado Sina Imani maana hii ya juu tu tayari Ina ufaView attachment 2123224
Amina Asante. Nimepata wazo la kumtafuta mtaalam Kwanza nimpeleke akanishaur. Nikiona Mambo yatakuwa mengi Sana nitauza nikanunue kwingine kusiko na changamoto hiyoHujachemsha mkuu,, Leveling uliyofanya si umejaza upande mmoja ambao kama ungejenga kawaida huo upande msingi ungekuwa mrefu kidogo....
Kama nature ya eneo ilikuwa na mwinuko sana huna namna,,, hapo lazima msingi uwe kama nyumba nyingine (idadi ya tofali za msingi inaweza kuwa sawa na tofali za kupandisha)....
Jipe muda na fanya maamuzi sahihi,,, Kosa la kwanza sio kosa,, ila kurudia kosa ni kuonyesha kwamba hutaki kujifunza, na Dunia itakufunza zaidi kwa Vitendo..
Kila la heri liwe upande wako ufanikishe Ujenzi.
Ukifikia kwenye umeme tutaftane bossMimi Ni Dada. Asante nitakutafuta kwa ushaur
Kujenga kwenye viwanja vya mtelemko ni gharama sana.
Kuliko kumwaga kifusi, bora ungechimba usawazishe tuHabar zenu. Nimefanya leveling mwez January mwaka huu kwenye kiwanja kilichokuwa na mteremko. Kama haitoshi nimemwaga vifusi kadhaa vya udongo ili kusawazisha kiwanja kile kwan hata baada ya kulevo Bado mteremko uliendelea kuwepo .
Kwa wazoefu na wajuzi Ni muda gani mzuri naweza kuanza ujenzi na kusiwe na athar za kutitia kwa jengo?
Mbona kujenga simpo, ww unataka nyumba ya room ngap?Huwa nikiwapa watu Bajeti ya msingi wangu wananiona mkatishaji tamaa