Leveling na kuanza ujenzi

Naona nimeshakosea. Napaswa kupasahau kidogo ili nifanye Mambo mengine. Au kuamua alternative nyingine ya kupauza kabisa nikatafute kwingine
 
Naona nishachemsha. Inabid nijipe muda wa kutafakar nione Cha kufanya Kama Ni kuuza au kuvumilia huku nikifanya shughul nyingine
 
Ulifanya kuosa, ungetafuta wataalamu wa ujenzi wangekusaidia sana. Pia punguza gharama kwa kujenga kutokana na eneo lilivo. Unaweka steps tu
Sikufikiria vizur ndugu yangu. Nishakosea
 
Daah. Umekosa sana mkuu. Hizo gharama za levelling bora ungeingia gharama kunyanyua msingi tu. Nimefanya kama ulivyofanya wewe ila ni baada ya kujenga nyumba ndogo na kuacha matolea. Kwa Sasa imepita miaka mitatu ila bado Sina Imani ya kuvuta hii nyumba. Nawaza kupiga underground tu

Ukiangalia huku nyuma niliacha matoleo lengo ni kuja kuweka sebule, dining, Jiko na vyoo ila bado Sina Imani maana hii ya juu tu tayari Ina ufaView attachment 2123224
 
Naona nishachemsha. Inabid nijipe muda wa kutafakar nione Cha kufanya Kama Ni kuuza au kuvumilia huku nikifanya shughul nyingine

Hujachemsha mkuu,, Leveling uliyofanya si umejaza upande mmoja ambao kama ungejenga kawaida huo upande msingi ungekuwa mrefu kidogo....

Kama nature ya eneo ilikuwa na mwinuko sana huna namna,,, hapo lazima msingi uwe kama nyumba nyingine (idadi ya tofali za msingi inaweza kuwa sawa na tofali za kupandisha)....

Jipe muda na fanya maamuzi sahihi,,, Kosa la kwanza sio kosa,, ila kurudia kosa ni kuonyesha kwamba hutaki kujifunza, na Dunia itakufunza zaidi kwa Vitendo..

Kila la heri liwe upande wako ufanikishe Ujenzi.
 
Picha haifunguki. Ila Asante kwa maelezo
 
Amina Asante. Nimepata wazo la kumtafuta mtaalam Kwanza nimpeleke akanishaur. Nikiona Mambo yatakuwa mengi Sana nitauza nikanunue kwingine kusiko na changamoto hiyo
 
Nilipewa kiwanja na bi. Mkubwa ambao una mtelemko, ujenzi wa msingi peke yake ambao upande wa mtelemko lazima ujenge underground uligharimu Tsh. Milioni saba na something. Nyumba ni ya vyumba viwili, sebule, jiko na vyoo viwili master na kawaida. Ukichanganya na kile chumba cha underground unapata vyumba vitatu maana ni chumba kilichokamilika kabisa mtu anaweza kuishi. Hizi gharama nilizotumia za msingi ingekuwa kiwanja cha tambalale ningenyanyua pagale kabisa. Kujenga kwenye viwanja vya mtelemko ni gharama sana.
 
Kuliko kumwaga kifusi, bora ungechimba usawazishe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…