Lexus is200 ina miss ikiwa katika neutral au parking tu

Lexus is200 ina miss ikiwa katika neutral au parking tu

I think itakuwa inayo nne, mbili kwenye manifold, moja before cat na nyengine after cat. Niko mbali na gari yangu, mpaka nikienda tena garage (jumatano tena, coz nafanya kazi shamba and j5 ndo day off) Nitacheki tena with diagnosis kutizama ni Sensor ipi hio inapata mushkel.....

Mimi nimetaka kuagizia SPacer kuifunga na hio sensor
 
Sasa mjomba gari Ina matatizo unakuja jamii forums,are u kidding
Mjomba nimekuja jamii forum kupata ushauri, mbona hii ni kawaida tu. Unaweza ukampelekea fundi tatizo ambalo hajawahi kukumbana nalo, lakini humu ukakuta tayari kuna mtu analijua ufumbuzi wake akakupa idea. Gari nishampelekea fundi na tumebadilisha coil zote sita na plug zote sita, yaani imecost bei ya engine nyengine tena lakini bado.

Ninaweza nikaendesha ivi ivi kwa sababu tatizo linakuja gari ikikaa silence kwa mda, fuel economy haijachange ipo kawaida while driving, hakuna chochote ambacho kinafail kwa sababu ya hili tatizo, ila inankera upumuaji wake, sio smooth.
 
Vipi taa ya check engine inawaka continuosly?
 
Vipi taa ya check engine inawaka continuosly?
Mkuu haizimi hio, yaani kuizima kwake ndo kama ivo ufanye kwa kuchomoa betry, tena ukirudisha betri baada ya mda tena inajirudi
 
Habari wadau,

Gari yangu imekuwa ina act kiajabu kidogo. Inamiss ikiwa umepark au ipo katika neutral, na hii hutokea either ikiwa imekaa silence kwa mda kidogo japo dakika 5 ivi ndo inaanza hii kitu. Sasa nimefanya engine diagnosis imetokea code inanambia oxygen sensor imebuma/au haipeleki data sawasawa. Nilimpelekea fundi amaeitizama kwa macho na amenambia inaonekana kama engine inashindana na choke, kana kwamba choke inakuwa activated pale inapoonekana engine inapoteza nguvu kisha ikirudi ina deactivate lakini ina activate tena kwa sababu engine bado inapoteza nguvu. Nimejaribu kufanya tena diagnosis imekuja same problem ya O2 sensor.

Nimebadilisha all 6 coils, na nimereplace all spark plugs nimeweka iridium spark plugs mpya, hii ngoma bado inanletea ubishi. Kwanini sikubadilisha hio sensor? Ni kwa sababu niliamini kuwa hizo bad readings ni kwa sababu nimechana ile catalytic convertor!!!! nili install custom exhaust sasa nilichana hio catalytic (ule mtungi wa chini baada ya manifold).

Sasa nimefanya research nafikiri itanilazima kubadili hio sensor tu sasa. Lakini nina wasiwasi pengine my sensor is working fine ila kwa sababu nimekata hio catalytic convertor inapeleka fixed readings (open loop) na sio dynamic readings (closed loop) na kusababisha engine ku loose power ikiwa in silence. Katika research, hii copmuter ya hii gari na hizi sensor huwa zina fixed data just in case ikiwa inapeleka wrong readings wakati. Sasa wakuu hapa nkibadilisha sensor si itakuwa ndo yale yale kutia maji kwenye pakacha? solution hapa ni nini? nimesikia kuna spacer unaweka na hio sensor kwaio sensor itaidanganya computer.

Msaada wakuu
Mkuu umetisha sanah na hayo maelezo.. Me najua kubadilisha tairi tu.. Hehehe tenah la baiskeli
 
Mkuu umetisha sanah na hayo maelezo.. Me najua kubadilisha tairi tu.. Hehehe tenah la baiskeli
Mkuu mi mwenyewe zamani nlikuwa kama wewe tu, ila mi nkawa mbishi, nikipeleka chombo gereji sitoki, nakodoa macho na kuuliza maswali kwa mafundi. Nikiona tatizo linasumbua sana najitosa google kwenye forums za gari husika ili kujifunza common problems. Halafu nimekuwa na intrest sana na car tuning na perfomance mods, ila mda na mwalimu sijapata. Kabla hujenda kwa mafundi ukiona tatizo ni vema ukagoogle ukaona maoni ya watu wengine, ukienda garage na wewe una dadisi kidogo una gain knowledge. Ishu ndogo ndogo unaweza ukajua tatizo ni nini.
 
Naamini Lexus ni brand ya Toyota, hivyo unaonaje ukilipeleka gari lako Toyota Tanzania ili waliangalie na kurekebisha hio kasoro? Au wao hawana huo utaalamu?
akifika toyota hawanaga kuumiza kichwa wao ni wafanya biashara tuu .watakachokifanya nikumwagizia cat nyingine
 
akifika toyota hawanaga kuumiza kichwa wao ni wafanya biashara tuu .watakachokifanya nikumwagizia cat nyingine
kweli mkuu, afu toyota wa kwetu wangu ukimtajia lexus tu bei zinabadilika wakati ni same engine
 
akifika toyota hawanaga kuumiza kichwa wao ni wafanya biashara tuu .watakachokifanya nikumwagizia cat nyingine
Aaaaha, kazi ipo, nadhani na uhindi uhindi unakuwa mwingi sana.
 
Wacha kesho niende garage nimsikilize fundi anaendeleaje
 
Back
Top Bottom