Lexus is200 ina miss ikiwa katika neutral au parking tu


Mimi nimetaka kuagizia SPacer kuifunga na hio sensor
 
Sasa mjomba gari Ina matatizo unakuja jamii forums,are u kidding
Mjomba nimekuja jamii forum kupata ushauri, mbona hii ni kawaida tu. Unaweza ukampelekea fundi tatizo ambalo hajawahi kukumbana nalo, lakini humu ukakuta tayari kuna mtu analijua ufumbuzi wake akakupa idea. Gari nishampelekea fundi na tumebadilisha coil zote sita na plug zote sita, yaani imecost bei ya engine nyengine tena lakini bado.

Ninaweza nikaendesha ivi ivi kwa sababu tatizo linakuja gari ikikaa silence kwa mda, fuel economy haijachange ipo kawaida while driving, hakuna chochote ambacho kinafail kwa sababu ya hili tatizo, ila inankera upumuaji wake, sio smooth.
 
Vipi taa ya check engine inawaka continuosly?
 
Vipi taa ya check engine inawaka continuosly?
Mkuu haizimi hio, yaani kuizima kwake ndo kama ivo ufanye kwa kuchomoa betry, tena ukirudisha betri baada ya mda tena inajirudi
 
Mkuu umetisha sanah na hayo maelezo.. Me najua kubadilisha tairi tu.. Hehehe tenah la baiskeli
 
Mkuu umetisha sanah na hayo maelezo.. Me najua kubadilisha tairi tu.. Hehehe tenah la baiskeli
Mkuu mi mwenyewe zamani nlikuwa kama wewe tu, ila mi nkawa mbishi, nikipeleka chombo gereji sitoki, nakodoa macho na kuuliza maswali kwa mafundi. Nikiona tatizo linasumbua sana najitosa google kwenye forums za gari husika ili kujifunza common problems. Halafu nimekuwa na intrest sana na car tuning na perfomance mods, ila mda na mwalimu sijapata. Kabla hujenda kwa mafundi ukiona tatizo ni vema ukagoogle ukaona maoni ya watu wengine, ukienda garage na wewe una dadisi kidogo una gain knowledge. Ishu ndogo ndogo unaweza ukajua tatizo ni nini.
 
Naamini Lexus ni brand ya Toyota, hivyo unaonaje ukilipeleka gari lako Toyota Tanzania ili waliangalie na kurekebisha hio kasoro? Au wao hawana huo utaalamu?
akifika toyota hawanaga kuumiza kichwa wao ni wafanya biashara tuu .watakachokifanya nikumwagizia cat nyingine
 
akifika toyota hawanaga kuumiza kichwa wao ni wafanya biashara tuu .watakachokifanya nikumwagizia cat nyingine
kweli mkuu, afu toyota wa kwetu wangu ukimtajia lexus tu bei zinabadilika wakati ni same engine
 
akifika toyota hawanaga kuumiza kichwa wao ni wafanya biashara tuu .watakachokifanya nikumwagizia cat nyingine
Aaaaha, kazi ipo, nadhani na uhindi uhindi unakuwa mwingi sana.
 
Wacha kesho niende garage nimsikilize fundi anaendeleaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…