Mashamba Makubwa Nalima
JF-Expert Member
- Mar 19, 2024
- 4,978
- 2,411
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kumchukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kutokana na kauli yake anayodaiwa kuitoa hivi karibuni ambayo wamedai kuwa inatweza utu wa Mwanamke.
Aidha kufuatia kauli hiyo, LHRC kupitia Mkurugenzi Mtendaji, Dr. Anna Henga wametoa wito kwa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma kumuita na kumuhoji Chalamila kufuatia kauli yake.
Itakumbukwa hivi karibuni Chalamila alinukuliwa kupitia picha mjongeo akitoa kauli ambayo iliibua gumzo mtandaoni kuhusu Mwanamke ambaye alimpigia akiwa hospitalini kuhoji gharama za kujifungua alizotakiwa kulipia.
Soma: RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani