Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kumchukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kutokana na kauli yake anayodaiwa kuitoa hivi karibuni ambayo wamedai kuwa inatweza utu wa Mwanamke.
Aidha kufuatia kauli hiyo, LHRC kupitia Mkurugenzi Mtendaji, Dr. Anna Henga wametoa wito kwa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma kumuita na kumuhoji Chalamila kufuatia kauli yake.
Itakumbukwa hivi karibuni Chalamila alinukuliwa kupitia picha mjongeo akitoa kauli ambayo iliibua gumzo mtandaoni kuhusu Mwanamke ambaye alimpigia akiwa hospitalini kuhoji gharama za kujifungua alizotakiwa kulipia.
Nilidhani LHCR wataanzisha uchunguzi WA kwanini hospitali hazina vifaa!
Pumbavu zenu, ulizeni serikali fungu la pesa za basket fund kwanini zimepungua kwa zaidi ya asilimia 60 tangu awamu hii imeingia madarakani? Ulizeni pesa za uchangiaji wa matibabu kwenye vituo vya serikali mbona zina mlolongo mrefu wakati vituo vikiomba kuzitumia kunulia vifaa tiba vya dharula....
Baada ya Chalamila kujikanyaga na kusema kuwa Wajawazito wanaogoma kununua gloves wakajifungulie nyumbani watu wamechachamaa
---------------------------------------------------------------
Your browser is not able to display this video.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekemea vikali kauli ilizozitaja kuwa za
udhalilishaji na zinazotweza utu wa mwanamke zinazodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, wakati wa hafla ya hadhara iliyofanyika wilayani Temeke, Dar es Salaam.
LHRC imetoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Albert Chalamila kwa kauli zake zilizotajwa kuwa za udhalilishaji. Pia, LHRC imeitaka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kumhoji Chalamila iwapo hatua za kinidhamu hazitachukuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kuacha kuingiza siasa katika mambo yanayowahusu binafsi hasa katika Afya kwani hazitawasaidia badala yake zitawachelewesha na pia kuwa na madhara zaidi. Akizungumza hivi karibuni na wanachi wa Temeke jijini Dar Es...
Mkuu huwezi kuwa kiongozi ukawa unatoa majibu ya ovyo hivyo. Wengine watajifunza kwake
Kauli zake nyingi anazotoa ni kama he is doing us a favor au kalazimishwa aongoze
Kazidisha sifa hadi ana haribu sasa
Mkuu huwezi kuwa kiongozi ukawa unatoa majibu ya ovyo hivyo. Wengine watajifunza kwake
Kauli zake nyingi anazotoa ni kama he is doing us a favor au kalazimishwa aongoze
Kazidisha sifa hadi ana haribu sasa
Mkuu huwezi kuwa kiongozi ukawa unatoa majibu ya ovyo hivyo. Wengine watajifunza kwake
Kauli zake nyingi anazotoa ni kama he is doing us a favor au kalazimishwa aongoze
Kazidisha sifa hadi ana haribu sasa
Mkuu huwezi kuwa kiongozi ukawa unatoa majibu ya ovyo hivyo. Wengine watajifunza kwake
Kauli zake nyingi anazotoa ni kama he is doing us a favor au kalazimishwa aongoze
Kazidisha sifa hadi ana haribu sasa
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinasikitishwa na kauli za kufedhehesha na kutweza utu wa mwanamke na kauli nyingine za kutatanisha zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa umma kinyume na maadili na miiko ya utumishi wa umma, haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Mkuu alitakiwa ashtakiwe kwa uchochezi. Mbona viongozi wa upinzani wanashtakiwa kwa kutoa kauli za uchochezi na ukizisikia hazina utofauti na za huyu Mkuu wa mkoa wa Dar.