06 September 2021
Morogoro, Tanzania
LHRC YAWASILISHA RIPOTI YA UTAFITI WA SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI NA UHUJUMU UCHUMI, YALIA
WASHIRIKI kutoka taasisi za Serikali, viongozi, wahadhiri vyuo vikuu UDSM na UDOM, Asasi za Kiraia, walimu wa vyuo vikuu pamoja na waandishi wa habari wameshuhudia uwasilishwaji wa Ripoti ya Utafiti wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura Na. 20 pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi sura no. 200.
Wakili Anna Henga mkurugenzi wa LHRC wametafiti mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa dhamana toka mwaka 1945 - 2021. Zanzibar makosa yote yana dhamana kwa tuhuma zote. Kunyimwa dhamana ni sawa na kuhukumiwa kabla hata kesi kusikilizwa.
Nchi za Zanzibar, Malawi, Kenya, Zambia na Uganda zilifanyiwa rejea kama nchi za Jumuiya za Madola / Commonwealth katika kongamano hilo lililofanyika mjini Morogoro Tanzania kuhusu makosa gani Mahakama inaweza kutoa dhamana na siyo Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu DPP .
Kesi ya Mutobesya mahakama...
Source: MwanaHALISI TV
Soma zaidi kwa kina :

LHRC yaomba maboresho sheria ya makosa ya jinai
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kimesema sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ambayo imefanyiwa marekebisho Mwaka 1985 kwa kuondoa kifungu kinachoipa mahakama kuu kutimiza maombi ya dhamana hata katika makosa yasiokuwa na dhamana imepelekea mtuhumiwa kupewa dhamana kama anapewa zawadi badala ya haki.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Kituo cha sheria na haki za binaadamu nchini Tanzania Wakili Ana Henga, Mjini Morogoro Septemba 6, 2021 wakati akifungua kikao kazi cha wadau kwaajili ya kutoa wasilisho la ripoti ya makosa yasiyo na dhamana.
Wakili Ana Henga amesema ni wakati muafaka wa nchi ya Tanzania kuweka maboresho ya mfumo wa dhamana kutokana na mfumo uliopo sasa kuminya haki za Binaadamu na kumuumiza mtu kimwili na kisaikologia.
Aliongeza kuwa kituo cha sheria na haki za binaadamu (LHRC) kiliangalia mfumo wa utoaji haki ya dhamana hapa nchini kwa kipindi cha mwaka 1945 hadi 2021 kuwa sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1945, ambapo iliipa mamlaka mahakama kuu kusikiliza maombi ya dhamana hata katika makosa yasiyo na dhamana.
“sheria hii ilidhihirisha kwa vitendo dhamana ya uhuru pamoja na dhana yakutokuwa na hatia hadi pale mahakama itakapothibitisha hivyo katika kipindi cha kuanzia mwaka 1945 hadi 1984 mahakama kuu ilikuwa na uwezo huo katika makosa yasiyo na dhamana , kwa bahati mbaya sheria na mwenendo wa makosa ya jinai 1985 iliondoa kifungu kilichoipa mahakama mamlaka hiyo hivyo kwa sasa mtu atakaye tuhumiwa na kosa lisilo na dhamana uhuru wake unapokonywa mpaka kesi yake itakapo hitimishwa na mahakama”.Amesema Wakili Henga
Aidha alisema utafiti huo uliofanywa na LHRC ulifanya ulinganifu wa mfumo wa utoaji haki katika nchi tano (5) za kenya , uganda, malawi , zambia na Zanzibar.
“Niseme tu kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka katika mifumo ya nchi za jirani ili kuboresha mfumo wetu na ni imani yetu kwamba mkutano huu utachochea mabadiliko na hoja zenye uzito baada ya kupata mwanga wa kufahamu kwa kina kutoka wasilisho la leo.” Amesema Ana Henga
Henga ameongeza kuwa mchakato wa upatikanaji haki kupitia mfumo uliopo sasa wa haki ya jinai unapingana na dhana iliyopo nchini ya ibara ya 13 (6)b ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayoweka dhana ya msingi ya kutokuwa na hatia hadi mahakama itakapothibitisha. Source : LHRC yaomba maboresho sheria ya makosa ya jinai - 2 Eyez Media