Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumzia ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga, Juni 13, 2024 alisema uchambuzi ulionesha katika takwimu hizo Wanawake walikuwa manusura wakuu kwa asilimia 56, ikilinganishwa na Wanaume walio na asilimia 44.
Mkurugenzi huyo amesema licha ya mafanikio hayo katika kuripoti matukio kupitia mfumo huo wa Kidigtali, anadai bado kuna vikwazo mbalimbali ambavyo vimekuwa vikiwaweka mbali Wanawake kwa muda mwingi katika matumizi ya vifaa vya Kidigtali, ikiwemo muda mwingi kuhusika katika shughuli za malezi Kifamilia.
Aidha, aliongeza kuwa katika masuala yaliyofuatiliwa na Kituo hicho asilimia 12 yametatuliwa katika ngazi mbalimbali.
"Takriban asilimia 12 ya masuala yamefanikiwa kutatuliwa, yakihusisha ngazi za familia, polisi na mahakama. Karibu asilimia 29% ya kesi zilielekezwa kwa msaada wa kisheria, hususani kwa msaada wa kisheria kwa uwakilishi wa mahakamani au kuwawezesha kujitetea wenyewe, hasa katika masuala yanayohusiana na ardhi,” alisema Henga
Lakini pia Ripoti hiyo inaonesha kuwa katika kipindi cha utekelezaji, wameona ufanisi katika Uwajibikaji wa makampuni ambayo kituo hicho kilifanya nayo kazi, hasa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, kufuatia mapendekezo ya viwango vya Haki za Binadamu.
Henga amesema maendeleo hayo ni matokeo ya ushirikiano na mgodi kuhusu jinsi ya kufuata viwango vya haki za binadamu kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.