LHRC, Sheikh Ponda wataka uchunguzi wa kina kifo cha mtuhumiwa wa ugaidi anayedaiwa kufia kwenye mikono ya Dola

LHRC, Sheikh Ponda wataka uchunguzi wa kina kifo cha mtuhumiwa wa ugaidi anayedaiwa kufia kwenye mikono ya Dola

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), wametaka ufanyike uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha kifo cha marehemu Sheikh Said Mohamed Ulatule ambaye anadaiwa kufia gerezani akiwa anatuhumiwa na makosa ya Ugaidi.

Wito huo ambao umetolewa leo Machi 15, 2023 na Mkurugezi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Sheikh Ponda Issa Ponda, wamesema kuwa uchunguzi huo ufanyike na ukawe endelevu kwa watu wote wanaopoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyombo vya Dola.

"Ufanyike uchunguzi wa kina (inquest) juu ya nini hasa chanzo cha kifo cha marehemu Sheikh Said Mohamed Ulatule na utaratabu huo uendelee kwa watu wote wanaopoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo Sura ya 24 ya mwaka 1980 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019" amesema Mkurugezi Mtendaji LHRC, Anna Henga.

Kwa upande wa Sheikh Ponda amesema kuwa taarifa za kifo hicho zinaibua maswali mengi kwa wadau wa haki pamoja na familia ya marehemu, hata hivyo amedai kuwa watuhumiwa wengine zaidi ya 100 wanaokabiliwa na mashtaka ya Ugaidi Bado wapo kwenye magereza tofauti Nchini kwa miaka sita hadi 10 na kuwa hatma yao haijulikani.

Katika wito huo wamedai kuwa ni jambo la kushangaza kuona watuhumiwa wanakaa gerezani kwa kipindi cha mika sita na zaidi bila uchunguzi wa kesi zao kukamilika kama inavyoelezwa na upande wa mashtaka.

Aidha kufuatia jambo hilo wameitaka ofisi ya Taifa ya mashtaka chini ya DPP, kuwafutia mashtaka watuhumiwa au kuhakikisha wanapeleka uchunguzi mahakamani ili haki iweze kutendeka kwa mujibu wa Sheria.

Sanjali na hoja hizo Wakili Anna Henga amesema kuwa hawaungi mkono vitendo vya ugaidi bali wanachosisitiza ni haki kutendeka kwa watuhumiwa sio kutumia tuhuma hizo kuwakosesha haki muhimu.

Ikumbukwe ilidaiwa kuwa Sheikh Saidi (80) aliyekuwa akituhumiwa kwa kesi ya ugaidi akishikiliwa kwenye mahabusu ya Gereza Kuu la Ukonga, jijini Dar es Salaam alianguka na kufariki akiwa mbele ya Mh. Jaji . Tukio hilo lilidaiwa kutokea March 4, 2023.

Taarifa ya awali iliyodaiwa kutolewa Jumanne, Machi 7, 2023 na Katibu Mkuu wa Shuraa ya Maimamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, zinaeleza kuwa Sheikh Ulatule, alifariki dunia mbele ya Jaji huyo Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, tarehe 4 Machi 2023.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe huyo mlalamikaji bado yupo?! 😳😅😅😅

Mbona hakusikika awamu ya Tano?! 😅
 

15 March 2015​

LHRC kwenda kwa Rais Samia sakata la mashekhe wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi​



PONDA-1024x638.jpg

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), kimesema kina mpango wa kwenda kwa Rais Samia Suluhu, kuwasilisha ombi la kufanyiwa kazi mashauri yaliyokaa muda mrefu kwa kigezo cha Jamhuri kutokamilisha upelelezi wake, ikiwemo mashtaka ya ugaidi yanayowakabili masheikh na wafuasi wao zaidi ya 100.


Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga, leo amewaambia wanahabari kwamba mashauri hayo ya ugaidi yamekwama kuendelea kwa zaidi ya miaka sita kutokana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kutokamilisha upelelezi wake.

“Tuna mpango wa kwenda kumuona waziri mhusika, ikiwezekana kwa Rais kuhusu hili suala ili kuhakikisha hawa watu haki zao zinapatikana aidha kwa kusikilizwa kama kuna ushahidi au kuachwa huru kama hakuna ushahidi,” amesema Henga.


Katika hatua nyingine, Henga ameitaka Ofisi ya Mwendesha mashtaka nchini, awafutie mashtaka kama hakuna ushahidi au awafikishe mahakamani watuhumiwa hao kwa ajili ya kupata haki yao ya kujitetea kwa mujibu wa sheria.


Wito huo wa LHRC umejiri ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Sheikh Said Ulatule, afariki dunia kwa matatizo ya moyo, akiwa mahabusu ya Gereza la Ukonga, akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi kwa zaidi ya miaka sita.

Henga, ameshauri uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini kiini zaidi cha chanzo cha kifo chake.

Naye Katibu wa Jumuiya za Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameiomba Serikali ifanyie kazi suala hilo, ili watuhumiwa wapate haki yao, ambapo amesema katika mahabusu ya Gereza la Ukonga wako watuhumiwa wa ugaidi 70, wakati mkoani Tanga wakiwa 23, huku mahabusu ya Gereza la Kisongo Arusha wakishikiliwa 23 na Morogoro wakishikiliwa 21.

Amesema mbali na idadi hiyo, bado wengine wako katika mahabusu za magereza ya mikoa mbalimbali, ikiwemo mwanza na Tabora.

Mohamed Ulatule, mtoto wa Sheikh Ulatule aliyefariki dunia mahabusu, ameiomba Serikali itende haki kwa wanafamilia wengine sita waliosalia mahabusu, akiwemo kiongozi wake, Mzee Suleiman Ulatule (96), Ali Ulatule (75), Khamis Ulatule (61) na Ramadhani Ulatule, ambao wanashikiliwa kwa tuhuma za mahabusu tangu 2017.

Mohamed amedai kuwa, tangu wanafamilia hao washikiliwe, familia yake inakumbana na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuwalea na kusomesha watoto wao.
 
22 December 2024

Mzee wa miaka 99 afia gerezani na ujumbe kwa Rais Samia | GUMZO MAALUM | Sheikh Ponda & M.Ghassani



View: https://m.youtube.com/watch?v=ArdvNBip-3I
Shahidi Sheikh Suleiman Mohammed Abdallah Ulekule amerejea kwa Mola wake akiwa na umri wa miaka 99 akiwa gerezani alikokaa kwa miaka tisa, tangu yeye na watu 15 wa ukoo wake walipokamatwa mwaka 2015.

Sheikh Suleiman Mohammed Abdallah Uletule amefariki dunia mwaka mmoja baada ya ndugu yake mwenye umri wa miaka 79 naye kutangulia mbele ya haki akiwa pamoja naye gerezani. Sheikh Ponda Issa Ponda amekuwa akiwahangaikia ndugu hao kwa muda wote tangu wamepatwa na balaa hili.
 
Back
Top Bottom