Harvey Specter
Member
- Jun 26, 2024
- 41
- 57
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) imeripoti kuwa imekua ikipokea na kufuatilia taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu zinazohusisha kushikiliwa kwa wananchi kwa muda mrefu bila dhamana au kufikishwa mahakamani katika maeneo mbalimbali nchini.
Imeripoti kwamba mkoani Shinyanga, zaidi ya wananchi 200 kutoka Kata ya Idukilo, Wilaya ya Kishapu, wanadaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa zaidi ya siku sita bila kufikishwa mahakamani. Pia imetaarifu Umma kwamba imepokea taarifa za madai ya vipigo vilivyofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga pamoja na uharibifu wa nyumba na maduka ya wananchi.
Mkoani Morogoro, wananchi wanne wa Kijiji cha Njiwa, Wilaya ya Malinyi, wanashikiliwa tangu tarehe 3 Juni 2026 bila dhamana wala kufikishwa mahakamani kufuatia mgogoro unaohusiana na utendaji wa uongozi wa kijiji.
Aidha, Mkoani Singida, watumishi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wanaripotiwa kushikiliwa kwa takribani siku nane bila kupewa dhamana au kufikishwa mahakamani huku tuhuma zinazowakabili zikiwa hazijawekwa wazi.
LHRC imezitaka mamlaka husika kuheshimu Katiba, sheria za nchi na misingi ya haki za binadamu kwa kuwaachia huru wanaostahili dhamana au kuwafikisha mahakamani mara moja ikiwa kuna tuhuma dhidi yao. LHRC isema taendelea kufuatilia kwa karibu matukio hayo na kuchukua hatua stahiki za kisheria ili kuhakikisha haki inatendeka.