LHRC Yafuatilia Wimbi la Malalamiko Kuhusu Uhaba wa Maji Safi na Salama Nchini

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinaendelea kufuatilia taarifa kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji. Taarifa zinazoendelea kuripotiwa zinaonesha kuwa wananchi wengi bado wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama pamoja na huduma zisizo za uhakika.

Maji ni hitaji la msingi kwa maisha, afya, usafi, na maendeleo ya jamii. Uhaba au kukosekana kwa huduma ya maji huongeza hatari ya magonjwa na kuwaathiri zaidi wananchi walio katika mazingira magumu, hususan wanawake na wasichana ambao mara nyingi hubeba jukumu la kutafuta maji kwa matumizi ya nyumbani. Hali hii pia huathiri upatikanaji wa elimu, usawa wa kijinsia, ustawi wa jamii, na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.

Licha ya kuwepo kwa miradi ya maji iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa, bado wananchi katika maeneo mengi wanaendelea kukabiliwa na changamoto za upatikanaji wa maji. Hivyo, kuna haja ya kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha kuwa miradi ya maji inaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi.
 
Nimewapigia home ,wanasema hawana maji siku ya tatu leo ,japo week iliyoisha mvua imepiga karibia siku tatu.

Bwawa la kidunda sijui litaisha lini.
 
Back
Top Bottom