LHRC yalaani tukio la Mdude Nyangali kuvamiwa, kuchukuliwa na Watu wasiojulikana

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2025-05-02 at 16.27.02_c463b38c.jpg

KUKEMEA NA KULAANI VIKALI SHAMBULIO DHIDI YA NDUGU MDUDE NYAGALI ​
Dar es Salaam, 02 Mei 2025

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinalaani na kukemea vikali shambulio dhidi ya ndugu Mdude Nyagali lililotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2025 akiwa nyumbani kwake mkoa wa Songwe. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la mashambulio dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu nchini yanayotekelezwa na watu wanaotambulika kama 'watu wasiojulikana'.

LHRC inalitaka jeshi la polisi mkoa wa Songwe kuchunguza kwa kina tukio hili na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa shambulio hili la kikatili. Jeshi la polisi Songwe pia litoe taarifa rasmi kwa umma kuthibitisha kutokea kwa tukio hili na hatua zilizochukuliwa hadi sasa.

Sambamba na hilo, LHRC inatoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba wa kufanya uchunguzi juu ya jambo hili na mengine ya namna hii yanayoendelea kuvunja haki za binadamu nchini.

Imetolewa na:
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Bw. Fulgence Massawe (Wakili)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.
 
Laana ya kushangilia kifo cha Magufuli ni kali...

Si Mbowe wala Lisu mwenye furaha kwa sasa
 
Ndio mdudu gani tena huyo? watu hawamjui. tufahamisheni ni nani?
 
View attachment 3322826

KUKEMEA NA KULAANI VIKALI SHAMBULIO DHIDI YA NDUGU MDUDE NYAGALI ​
Dar es Salaam, 02 Mei 2025

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinalaani na kukemea vikali shambulio dhidi ya ndugu Mdude Nyagali lililotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2025 akiwa nyumbani kwake mkoa wa Songwe. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la mashambulio dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu nchini yanayotekelezwa na watu wanaotambulika kama 'watu wasiojulikana'.

LHRC inalitaka jeshi la polisi mkoa wa Songwe kuchunguza kwa kina tukio hili na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa shambulio hili la kikatili. Jeshi la polisi Songwe pia litoe taarifa rasmi kwa umma kuthibitisha kutokea kwa tukio hili na hatua zilizochukuliwa hadi sasa.

Sambamba na hilo, LHRC inatoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba wa kufanya uchunguzi juu ya jambo hili na mengine ya namna hii yanayoendelea kuvunja haki za binadamu nchini.

Imetolewa na:
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Bw. Fulgence Massawe (Wakili)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.
Hili neno “wasiojulikana” walipendalo sana polisi ni intentionally misleading! Wale ni majambazi wa Serikali.

Siasa za matusi kama za Mdude mimi siziwezi. Bora nikaangalie challenge ya wimbo wa "KUNA" Tiktok
 
Back
Top Bottom