Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC) ni shirika la utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. LHRC ilianzishwa mwaka 1995 kama shirika lisilo la kiserikali, la hiari, lisiloegemea upande wowote na lisilo la faida, likiwa na madhumuni ya kufanya kazi ya kuwawezesha na kuhamasisha uelewa wa kijamii, wananchi wa Tanzania kuhusu haki za kisheria na za binadamu.
LHRC imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utawala wa kisheria wenye misingi ya kidemokrasia na unaozingatia haki za binadamu. Kumekuwapo na
chapisho mtandaoni likiwa na taarifa inayodai kuwa LHRC waliomba jeshi la polisi kulinda uchaguzi
CHADEMA.
Uhalisia wa taarifa hiyo ni upi?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa LHRC haikutoa taarifa ya kuliomba jeshi la polisi kulinda uchaguzi wa CHADEMA. Kurasa za mitandao ya kijamii ya
LHRC mnamo tarehe 21 Januari 2025 hazikuchapisha barua iliyo na taarifa hiyo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.
Aidha chapisho lilotumika kusambaza taarifa hiyo isiyo ya kweli, lilitumia utambulisho wa
Jamii Forums ambapo kurasa zake za mitandao ya kijamii hazikuchapisha taarifa hiyo kutoka tarehe tajwa.
Vilevile baadhi ya mapungufu yaliyopo yanabainisha kuwa taarifa hiyo ni ya kutengeneza, sehemu ya madhaifu hayo ni pamoja matumizi ya aina ya chapisho ambalo huwa halitumiki kwa ajili ya maudhui ya kisiasa, uwepo wa alama inayoonesha uwepo wa chapisho moja zaidi tofauti na uhalisia.
Si mara ya kwanza kwa wapotoshaji kupotosha taarifa kuihusu LHRC, tazama
hapa.