Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (
LHRC) ni shirika la utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. LHRC lilianzishwa mwaka 1995 kama shirika lisilo la kiserikali, la hiari, lisiloegemea upande wowote na lisilo la kibiashara, kwa lengo la kuwawezesha na kuwahamasisha wananchi wa Tanzania kuhusu masuala ya sheria na haki za binadamu.
Kituo hiki kimekuwa kikitoa msaada wa kisheria, kutetea na kulinda haki za binadamu, lakini pia kukosoa na kushauri endapo haki za binaamu zinaminywe.
Madai
Imezuka barua inayodaiwa kuwa imetolewa na Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) ikiwa na ujumbe wa kuwataka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kifuate sheria na kuheshimu haki za binadamu. Taarifa hiyo inaendelea kueleza kuwa katika siku za hivi karibuni chama hicho kimekuwa na mwenendo usioridhisha unaosharia uvunjifu wa amani. Barua hiyo imeambatanishw apia na grafiki inayofanana na chombo cha habari cha mtandaoni cha MillardAyo. Taarifa pamoja na barua hiyo imehifadhiwa
hapa na
hapa.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na kubaini kuwa madai
hayo si ya kweli. JamiiCheck imebaini kuwa barua hizo zinazosambazwa hazijatolewa na kituo cha sheria (LHRC) na haki za binadamu na hazipo katika
kurasa rasmi za mitandao ya LHRC.
JamiiCheck imefuatilia pia inayoonekana kuwa ni grafiki ya MillardAyo iliyokuwa na ujumbe unaosomeka
“LHRC Fateni sheria na kuheshimu haki za binadamu” na kubaini kuwa haijachapishwa na
MillardAyo. Aidha grafiki hiyo ina makosa ya kiuandishi mathalani imetumia neno
‘Fateni’ badala ya
‘Fuateni’.
JamiiCheck imewasiliana na LHRC ambao ndiyo wanaodaiwa kutoa barua hiyo, ambapo wamekanusha na kueleza kuwa;
"Barua hiyo haijatoka kwao imetengenezwa na watu wenye nia mbaya wenye lengo la kuwachafua."