LHRC yatoa wito Tanzania kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi kwa Watu Wote dhidi ya Kupotea na Kutekwa, 1994

LHRC yatoa wito Tanzania kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi kwa Watu Wote dhidi ya Kupotea na Kutekwa, 1994

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu kupotea kwa watu_page-0001.jpg

Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu kupotea kwa watu_page-0002.jpg

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WAHANGA WA MATUKIO YA KUTOWEKA NA KUTEKWA (ENFORCED DISAPPEARANCES)

Dar es Salaam, Agosti 30, 2024
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) leo Agosti 30, 2024 kinaungana na wadau wote wa Haki za Binadamu Duniani katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wahanga wa matukio ya kutoweka na kutekwa.

Tunaungana na Jumuiya ya Kimataifa kuwakumbuka wale wote waliotoweka na waliotekwa na familia zao ambazo zinaendelea kuteseka kutokana na matukio haya ya kikatili. Matukio ya utekaji ni moja ya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu. Matukio hayo yameacha familia za wahanga katika hofu kwa kutojua hatma ya wapendwa wao.

Hivi karibuni Tanzania imeshuhudia ongezeko kubwa la matukio ya watu kutoweka, aidha kwa kutekwa au kutoweka katika mazingira tatanishi pasipo kupatikana na wengine kupatikana wakiwa na majeraha makubwa huku baadhi ikipatikana miili yao ikiwa imetelekezwa.

Matukio haya yamezidi kuleta taharuki katika jamii zetu mpaka kusababisha vurugu na ukosefu wa amani katika baadhi ya maeneo nchini.

Ikumbukwe kamba, Umoja wa Mataifa uliadhimia na kupitisha Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi kwa Watu Wote dhidi ya Kutoweka, 1994.

Mkataba huu unaweka mfumo madhubuti wa kushughulikia ukiukwaji matukio ya utekekaji katika Jumuiya ya Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania.

Hata hivyo, Tanzania ikiwa mwanachama wa Jumuiya hiyo haijaridhia Mkataba huo ili kuufanya uwe sehemu ya sheria zake. Kufuatia ongezo la matukio ya utekaji nchini, ni sababu tosha ya kuifanya Tanzania kuridhia mkataba huo ili kuweka ulinzi thabiti kwa wananchi wake dhidi ya matukio hayo.

Kwa kuwa, Ibara 1 ya mkataba huo inabainisha na kuweka katazo la watu kuwekwa vizuizini na kutekwa kwa inakwenda kinyume na ulinzi wa Haki za Binadamu.

Pia, Ibara ya 2 inatafsiri vitendo vya kutoweka na utekaji ikijumuisha vitendo vya kukamatwa, kuwekwa kizuizini, kutekwa au namna yoyote ya kumnyima mtu uhuru iwe kwa kufanywa na Serikali, Vyombo vyake au kwa maelekezo ya Serikali kwa kuelekeza chombo au mtu huyo kuficha taarifa za alipo mtu aliyekamatwa au kutekwa.

Zaidi Ibara ya 3 na 6 ya Mkataba huo, inataka mamlaka kufanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki na kuwafikisha watu wote waliyohusika na matukio hayo ya kuficha taarifa za mtu aliyetekwa katika vyombo vya kisheria. Hata hivyo, Ibara ya 24 inaweka sharti kwa mamlaka husika zilizoridhia Mkataba huo kutoa fidia kwa wahanga wote wa matukio ya utekaji ikiwemo, kutoa fedha za matibabu, fidia ya madhira pamoja na huduma ya kisaikoloji kwa wahanga pamoja na familia zao,

Pamoja na ulinzi uliyowekwa na Ibara ya 14 pamoja na 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inalinda haki ya kuishi na uhuru wa mtu.

Katika kuadhimisha siku hii ya Kimataifa ya Wahanga wa Matukio ya Kutoweka na Utekaji na kukumbuka watu wote waliopotea na waliotekwa.

LHRC inatoa wito kwa serikali kama ifuatavyo;
1. Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi kwa Watu Wote dhidi ya Kupotea na Kutekwa, 1994 ili kukabiliana na ongezeko la matukio kupotea na kutekwa. Kwa kuwa Mkataba huu, umeweka taratibu madhubuti za ulinzi wa watu dhidi ya matukio utekaji. Hatua hii sio tu itaonesha kujidhatiti katika Jumuiya ya Umoja wa Kimataifa kudhibiti vitendo hivyo, bali pia itaongeza imani kwa wananchi wake juu ya ulinzi na usalama wao.

II. Serikali kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika ngazi ya jamii kwa kushirikiana na wananchi ili kudhibiti matukio hayo.

III. Serikali kupita vyombo vya ulinzi na usalama ifanye uchunguzi wa kina wa malalamiko dhidi ya matukio hayo hususani katika kipindi cha hivi karibuni. Kwa kuwa vitendo hivi vinaathiri zaidi watoto, wanawake na jamii yote kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom